Moto uliozuka
mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.
Moto
Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa
Libya na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa
kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kilkuwepo eneo la tukio na
kukuletea kila kilichojiri ,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda
waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa chanzo cha moto huo bado
hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kuhakikisha
amani na utulivu unakuwepo huku kikosi cha zimamoto na magari nayo
yaliendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja
wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea
kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo
hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.
Moto
huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na
baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Maalum
ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova amesema
vikosi vya uokoaji na Zima Moto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto
huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.
‘’Vikosi
vya zima moto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima na
uzimaji na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa’’amesema Kova.
Kova
amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa
ushirikiano ambavyo ni Zima moto za Uwanja wa Ndege,Zima Moto ya
Kampuni ya Ulinzi ya Altimate,Night Support ,pamoja na Kikosi cha Zima
moto ya Jiji.
Amesema
kuwa chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa.Amesema uchunguzi
wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea .Aidha Kamanda Kova
amesema thamani ya vitu vilivyoungua katika majengo hayo bado
wanaendelea na uchunguzi lakini hakuna maafa katika moto huo.
Naye
Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar
es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi
waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo
na wanaweza kuudhibiti.
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Libya na Moski.
Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.
No comments:
Post a Comment