Katibu wa Jumuiya ya wazazi katika chama cha mapinduzi CCM mkoa wa
Arusha Bi Anna Kiromo akipanda mti katika shule ya msingi mkombozi
ikiwa kama ni njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira ndani ya umoja huo.
(PICHA NA GLADNESS MUSHI WA -ARUSHA)
Mmoja wa viongozi katika chama hicho naye akiweka kumbukumbu ya mti katika eneo hilo la shule ya mkombozi kaloleni
NA GLADNES MUSHI- ARUSHA
VIONGOZI
wa dhebebu la Ah madiyya nchini wamewasihi waiislamu wenzao kote
nchini ,kuungana na kuomba dua la amani kuiombea nchi ili kuepusha
matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani , ambayo yamekuwa yakienda
kinyume na maandiko matakatufu yaliyopo kwenye Quran .
Wakizungumza
kwenye kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika
msikiti Ah madiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo ya mwenyezi
mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi ama mtu yoyote kutekeleza mauaji
dhidi ya waumini wa dini nyingine.
Kiongozi
mkuu mwenye cheo cha Amiri na mbashiri mkuu wa jumuiya ya waislamu wa
Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhly aliwaomba waislamu kote duniani
kuungana na kulaani vitendo vya kinyama vinavyofanyika kote duniani
hususani nchi chenye uislamu kwa madai ya kutaka haki.
Aliwaomba
watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na machafuko
mbalimbali yanayoendelea katika nchi za uislamu na kukilaani kikundi
kidogo wa wanamigambo cha Boko haramu nchini Nigeria, kinachotekeleza
mauaji kwa kisingizio cha kufuata maagizo ya uislamu yalioko kweneye
Quruan.
‘’sisi
waislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya
uvunjifu wa amani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini
wenzetu ,hakuna maandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini
nyingine ‘’alisema Choudhly.
Aidha aliongeza kwa kuwataka viongozi
wa madhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na
kujiepusha na uchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha
machafuko yanayoweza kuibuka.
Katika
hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo
madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi aliyeko
madarakani, badala yake watoe mchango wa kusukuma maendeleo ya taifa
hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine.
Naye
Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini,Mzafara Ahamad,alisema
kuwa lengo la kongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa
madhehebu mbalimbali ya dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba
amani .
Alisema
kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa
Ahmadiyya muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa
ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa upande wa sheikh mkuu wa Aha madiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu ya kuleta mitafaruku ya kidini.
Ameyasihi
madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba
amani ,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi
wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri
uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi.
Naye
meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasimi katika
kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa
kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo.
Aliwasihi viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.
A
normal girl from Newark, NJ who became the first ever female to break
the records in the charts, she made a breakthrough with such a VOICE
the world had never heard before, Whitney Elizabeth Houston, not her
colour, background, gender neither financial constraints could hold her
back, there is a LOT to be learnt from this ALL TIME LEGEND, a simple
mistake in life can have it all, she was among the most respectful,
beautiful, humble, no words could define her Amazing character that she
hold high attached to God's worship and praise, but sooner or later a
creature came into her life and all gone wrong, Whitney she lost it all
because she had true LOVE which unfortunately cost her lifetime, it is
a GREAT LESSON, she has left a LEGACY for all of us to learn from and
be more careful, more focused and on top off all not to sacrifice our
inner self and connection with Lord for the sake of a wicked soul, She
tried her best to find herself back but the wicked media which always
made infamous rants from her mistakes and staggering moments could not
let her to, perhaps it was too much for her to be able to hold onto
maybe, one thing for sure I know all Angels are beautiful but at least I
am sure for now not only when my day comes I will meet beautiful
Angels but also one with strikingly, amazingly, absolutely GREATEST
VOICE OF ALL TIMES, Whitney Elizabeth Houston
Mchezaji
Haroub Canavaro wa timu ya Yanga akijaribu kumzuia mshambuliaji wa timu
ya JKT Ruvu wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo jijini Dar es
salaam.
Mshabuliaji wa Yanga Davis Mwape ameipatia timu hiyo goli la kuongoza
lililodumu mpaka mpira ulipomalizika na kufanya na kufanya timu ya Yanga
kutoka kifua mbele kwa goli matokeo ya 1-0.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na Rais wa
Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa awamu
ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh
Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Mh Wilson Mkama kabla ya kuanza kwa
mkutano wa Halmashauri Kuu leo katika jengo la White House la Makao
Makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo February 12, 2012
Mdhamini
wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume
akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa
kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na
wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa
Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na
michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa
Yanga.
Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini katika
michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo akamuomba
mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo.
Mgeni
rasmi katika hafla ya timu ya Yanga kutimiza miaka 77 Dk Fenella
Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo
akizungumza katika hafla hiyo, huku Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga
akifurahia jambo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck
Sadik na kushoto ni mdhamini wa Yanga Mama Fatma Karume.
Katibu
Mkuu wa Yanga Selestini Mwesigwa akipiga mamombi kabla ya kuanza kwa
hafla hiyo kulia ni George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro na
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam Sadik Meck Sadik.
Ancle Hashim Lundenga kulia ndani kama unavyomuona akiwa ametulia kitini
Kutoka kulia ni Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic shabiki mkubwa wa Yanga Emmanuel Mpangala na Kocha msaidizi wa timu hiyo mwenye (Mzuka Mwingi) Fred Felix Minziro wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla hiyo.
· Yashusha Gharama za m-pesa kwa 75%
· Kiwango cha kuongeza salio kwa m-pesa nacho chaongezwa hadi 25%
Kampuni
ya huduma za simu za mkononi inayoongoza nchini leo imetangaza kwa
mpigo kwa wateja wake nchini jumla ya ofa 4 zitakazowafanya kuzidi
kufaidika, kuwezeshwa na kufurahia zaidi huduma za Vodacom m-pesa.
Wateja
wa m-pesa sasa wamepunguziwa gharama za kufanya miamala kupitia huduma
hiyo ambapo sasa kila muamala utagharimu Shilingi 50 ikiwa ni punguzo
la asilimia 75. Wakati huo huo Vodacom ikiongeza kiwango ambacho mteja
anaweza kununua muda wa maongezi kupitia huduma hiyo ya m-pesa hadi
asilimia 25 kutoka asilimia 10 ya sasa.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw.
Rene Meza amesema”Tunatambua ni kwa kiwango gani huduma ya m-pesa
imekuwa ya umuhimu kwa maisha ya kila siku ya Watanzania, hivyo ni jambo
la muhimu pia kwetu kuwapatia ofa zinazoakisi matumizi yao na
kuyafanya kuwa rahisi na nafuu zaidi.” “Hii ndio dira yetu kwa mwaka
huu na kuendelea” Alisema Bw. Meza.
Ofa
nyengine iliyotangazwa na kampuni ya Vodacom Tanzania ni inayomwezesha
mteja wa m-pesa sasa kuweza kutuma kiasi cha chini zaidi cha fedha cha
shilingi 500 kupitia simu yake ya mkononi. Bw. Meza ameielezea ofa hii
kuwa inalenga kuhakikisha kila Mtanzania bila kujali hali yake ya
kiuchumi anafaidika na huduma bora,salama, ya uhakika na kuaminika ya
m-pesa.
Aidha,
pamoja na ofa hizo, kampuni ya Vodacom imezindua pia promotion ya
m-pesa ambapo jumla ya Shilingi 480 Milioni zitashindaniwa na wateja
kadri ambavyo wanavyotumia huduma ya m-pesa.
Katika
promosheni hii wateja 100 watakuwa wakijishindia zawadi ya fedha
taslimu za kitita cha Shilingi 50,000 kwa kila mshindi kupitia droo
zitakazochezeshwa kila siku huku droo kuu ya kila mwezi kwa miezi mitatu
ikitoa mshindi wa Shilingi 10 Milioni. Promosheni hiyo itadumu kwa
siku tisini kuanzia Februari 13, mwaka huu.
“Dhamira
yetu ni ya dhati kuhakikisha wateja wetu wanakuwa na furaha wakati
wote na huku tukiwawezesha kadri wanayotumia huduma ya MPESA.
Tutaendelea kuboresha mfumo wa m-pesa sambamba na huduma zinazopatikana
katika MPESA ili izidi kuendana na mahitaji halisi ya maisha ya kila
siku ya wateja.” Alisema Bw. Meza.
Kupitia
huduma ya m-pesa mteja anaweza kufanya malipo kwa huduma mbalimbali za
kijamii ikiwemo kununua umeme – LUKU, kulipia DAWASCO na DSTV. Aidha
huduma ya m-pesa inaweza pia kutumika kulipia tiketi za usafiri wa ndani
wa anga kwa mashirika ya ndege ikiwemo Precision Air na Coastal Air,
kulipia ada za shule, kuweka na kutoa fedha katika akaunti ya benki ya
CRDB na huduma nyengine nyingi.
Hakuna
shaka huduma ya Vodacom m-pesa ndiyo huduma ya kibenki kupitia simu za
mkononi inayoongoza nchini ikiwa na mtandao mpana wa mawakala zaidi ya
18,000 walionena nchi nzima mijini na vijijini na inayokua kwa kasi.
Ubora na umashauri wa huduma hii unaifanya kampuni ya Vodacom kuzidi
kung’ara na kuongoza soko la huduma za simu za mkononi nchini.
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam lililochezwa Februari 11
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 67,548,000.
Jumla
ya watazamaji 19,257 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 117
kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP
A.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 10,303,932.20 kila timu ilipata
sh. 13,182,800.34, uwanja sh. 4,394,266.78.
Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,757,706.78, TFF
sh. 4,394,266.78, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,197,133.39, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 439,426.78 na
asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,394,266.78.
Gharama
za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000,
nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. wamuzi wa akiba sh.
30,000, tiketi sh. 4,350,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000,
umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina
(Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama
nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu
ilipata sh. 1,347,990,280 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) kilipata sh. 1,555,420.
Kamati
ya Ligi imeagiza mchezaji Patrick Mafisango wa Simba aandikiwe barua
ya onyo kutokana na kumsukuma mwamuzi Isihaka Shirikisho baada ya
kumuonesha kadi nyekundu mchezaji mwenzake Haruna Moshi kwenye mechi
kati ya Simba na JKT Oljoro.
Nayo
klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake
kurusha makopo ya soda na chupa za maji wakipinga uamuzi wa mwamuzi
Shirikisho kumtoa kwa kadi nyekundu Haruna Moshi.
Wachezaji
waliopigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja baada ya kuoneshwa kadi
nyekundu kutokana na kupiga ambapo pia wanakosa mechi tatu za ligi kwa
mujibu wa Kanuni ya 25 ni nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa na Cyprian
Lukindo wa Villa Squad.
Waamuzi
watatu na kamishna mmoja wameondolewa kuchezesha na kusimamia mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na kuonesha upungufu katika
uchezeshaji na usimamizi.
Uamuzi
huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Februari 11 mwaka
huu) ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za waamuzi na
makamishna wa VPL ambayo leo (Februari 12 mwaka huu) inaendelea katika
raundi ya 17.
Peter
Mujaya wa Mwanza aliyechezesha mechi namba 101 kati ya JKT Ruvu Stars
na Yanga amefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ya Ligi
Kuu ya Vodacom kwa kushindwa kumudu mchezo huo, hivyo kupata alama za
chini.
Naye
Isihaka Shirikisho wa Tanga ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa
VPL msimu huu kwa kushindwa kumudu mchezo namba 105 kati ya Simba na
JKT Oljoro. Moja ya udhaifu alioonesha ni kushindwa kumuadhibu mchezaji
Patrick Mafisango ambaye alimsukuma baada ya kumuonesha kadi nyekundu
Haruna Moshi wa Simba.
Mwamuzi
mwingine aliyefungiwa kwa miezi 12 kwa mujibu wa Kanuni ya 26(a) ni
Kennedy Mapunda wa Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 107 kati ya
Villa Squad na Simba. Moja ya udhaifu wa Mapunda ni kushindwa kumpa kadi
nyekundu Fred Cosmas wa Villa Squad baada ya kumuonesha kadi ya pili
ya njano.
Pia
waamuzi wasaidizi Michael Mkongwa wa Iringa na Kudura Omary wa Tanga
waliochezesha mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar wameondolewa
katika mechi zilizobaki za VPL kwa kutokuwa makini. Mwamuzi wa mechi
hiyo Ibrahim Kidiwa amepewa onyo.
Waamuzi
wengine waliopewa onyo na kutakuwa kujirekebisha ni Hashim Abdallah wa
Dar es Salaam aliyechezesha mechi namba 92 kati ya Moro United na
Yanga, na mwamuzi msaidizi wa mechi ya Simba na Coastal Union, Issa
Malimali wa Ruvuma.
Kamishna
wa mechi namba 112 kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Mohamed Nyange
ameondolewa katika orodha ya makamishna kwa mechi zilizobaki za VPL
kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Mwenyekiti
Msataafu CCM Ali Hassan Mwinyi amewataka wananchi wa Jimbo la Uzini
kutofanya makosa kumchagua Mgombea wowote wa Chama cha Upinzani badala
yake wamchague Mgombea wa CCM Mohammed Raza Daramsi ambaye ndiye
mgombea anayefaa kwa ajili ya maendeleo yao
Mwinyi
ameyasema hayo katika kiwanja za Manzese Uzini wakati alipokuwa
akifunga kampeni za CCM katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya
Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa Jimbo hilo
Amesema
Mohammed Raza ni Mpenda maendeleo na anayejali watu hivyo wananchi wa
Uzini wana kila sababu za kumchagua Mgombea huyo wa CCM ambaye
anawazidi sifa wagombea wote wa vyama vya upinzani
Ameongeza
kuwa kama watamchagua Raza matatizo ambayo yanalikabili Jimbo la Uzini
yatakuwa yamepata suluhisho la kudumu kutokana na dhamira ya dhati
iliyojengeka katika nafsi ya Mgombea wao na Chama chao
Ameyataja
matatizo ambayo yanalikabili Jimbo hilo kuwa ni pamoja na Maji Safi na
Salama, Elimu na Afya na kudai kuwa yanaweza kupata suluhu iwapo Raza
atachaguliwa
Mwinyi
ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amewasisitiza mamia ya wananchi hao waliohudhuria katika kampeni hizo
kutekeleza ahadi ya Chama kwa kumchagua Raza kama ambavyo Uongozi wa
CCM ulitekeleza ahadi ya wananchi hao kwa kumsimamisha mgombea huyo
ambaye alikuwa chaguo lao
Kwa
upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Balozi Seif Idd amewataka
wananchi hao kutochezea bahati waliyoipata ya kumchagua Raza kwani ni
mtu mwenye upendo na kuwajali wanyonge.
Mjumbe
huyo ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar amesema kuwa ikiwa
Raza ameweza kusaidia wananchi wa Majimbo mbali mbali wakiwemo wa Jimbo
lake hapana shaka Raza atakuwa na juhudi zaidi ya kuwasaidia wananchi
wake mwenyewe
Kwa
upande wake Raza amesema atahakikisha anawapatia maendeleo wananchi wa
Jimbo la Uzini pale watakapomchagua na kuweza kuwa nao kwa bega katika
kusimamia Ilani ya CCM
Amesema
Ilani ya CCM ndiyo ilani ambayo inatekelezeka kwa maendeleo ya
wananchi wa Jimbo hilo hivyo waendelee kumuunga mkono kwa kumpa kura
ambazo zitamfanya awe Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ili awatumikie
Wananchi
wa Jimbo la Uzini watapiga kura kesho kumchagua Mwakilishi wa Jimbo
hilo ambapo jumla ya Wagombea Watano wa Vyama mbali mbali vya siasa
nchini wanagombea nafasi hiyo iliyoachwa kufuatia kifo cha Mwakilishi
wa Jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment