TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, August 17, 2014

WANAOTUMIA MIZANI `FEKI` UNUNUZI WA PAMBA WAONYWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au  namba +255767869133.
Waziri wa Chakula, Ushirika na Masoko, Christopher Chiza
 
Wafanyabiashara ‘wanaochakachua’ mizani wakati wa ununuzi wa zao la pamba toka kwa wakulima katika mikoa ya kanda ya ziwa, wameonywa huku Wakala wa vipimo wakitakiwa kuwachukulia hatua wanunuzi hao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 11 wa wadau wa sekta ndogo ya pamba jijini Mwanza jana, Waziri wa Chakula, Ushirika na Masoko, Christopher Chiza, alisema kutokana na malalamiko ya mara kwa mara ya wakulima wa zao hilo, mamlaka ya vipimo isikwepe jukumu lake.

Aidha, Chiza alisema changamoto zinazowakabili wakulima zisiwe zile zile kila mwaka, bali lazima wajadili utatuzi wake badala ya kulalamikia matatizo.

Hata hivyo, alisema serikali inaendelea na juhudi za kuboresha chuo cha utafiti cha Ukirigulu ili kiweze kuwasaidia wadau wengi wa kilimo hicho.

Akizungumzia kampuni ya Quton inayodaiwa kutoa mbegu Uk 91 zenye manyoya na kuwapa hasara wakulima, Chiza alisema kampuni hiyo lazima ikae na wakulima ili kuwapa elimu kuhusiana na mbegu hizo.

Alisema kutokana na wakulima kupata hasara kupitia mbegu hizo, serikali imeamua kuwalipa fidia wakulima wa zao hilo katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Awali mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikillo, aliwahimiza wakulima wa pamba kuendelea kutumia kilimo cha mkataba kutokana na kuwa na faida.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba, Festus Limbu, alisema wakulima wa zao hilo wanakabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za mabadiliko ya mara kwa mara ya bei katika soko la dunia, pembejeo kutopatikana kwa wakati, wakulima kutegemea mvua, usimamizi hafifu na mfuko kuwa na madeni makubwa.
SOURCE: NIPASHE

No comments:

Post a Comment