Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
Na Mbeya yetu
Picha na Rashid Mkwinda Blog
WAKILI wa kujitegemea mkoani Mbeya na
mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa(MNEC) Sambwee Sitambala (42)amepandishwa kizimbani
katika mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi wilaya ya Mbeya akituhumiwa kwa makosa
mawili.
Shitambala amepandishwa leo akituhumiwa
kwa makosa ya kuingia kwa jinai na kujenga nyumba katika viwanja viwili namba
27 na 28 Block BB lililopo eneo la Gombe Uyole Jijini Mbeya.
Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi
mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, wakili wa serikali, Ahmed Stambuli, alisema kuwa
Shitambala anashitakiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai kinyume cha kifungu
namba 79 ya mwaka 2014 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Alisema kuwa mshitakiwa kwa nyakati
tofauti kati ya Juni 18, 2012 na Novemba 28, 2013 aliingia na kujenga katika
viwanja namba 27 na 28 ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali ya raia wa Tanzania
mwenye asili ya kiasia aliyefahamika kwa jina la Jaswinder Palsingh.
Alisema kulingana na mazingira hayo,
mshitakiwa amesababisha maudhi kwa mmiliki wa kiwanja hicho Palsingh na hivyo
kushitakiwa kwa kosa la jinai.
Shitambala ambaye alikuwa akitetewa na
Wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo Hakimu Ndeuruo
alisema kuwa dhamana ya Mshitakiwa iko wazi ikiwa atatimiza masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja na ahadi ya fedha kiasi cha sh. milioni 1.
Kwa upande wake wakili wa serikali
Stambuli alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba iko tayari
kuanza kusikilizwa na kuiomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi
hiyo.
Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo
hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.
Akizungumza nje ya mahakama mara baada
ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemtetea Shitambala,Luambano alisema
kuwa kesi hiyo imefika hapo kutokana na maslahi ya baadhi ya watu na kuwa
kisheria kesi za aina hiyo zinapaswa kusomwa katika mahakama ya Ardhi.
Alisema kuwa mteja amejenga katika eneo
ambalo wamejenga watu wengine wapatao 400 na kuwa hata hivyo kesi hiyo imemhusu
mteja wake pekee hali ambayo inaonesha nia mbaya iliyofanywa na mlalamikaji
dhidi ya mteja wake.
No comments:
Post a Comment