Waziri
wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Femella Mukangara (wa
pili kushoto) akiwasili katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi wakati wa
fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup yaliyofikia Tamati leo
kwa kuzikutanisha Timu za Temeke na Pwani.
Waziri
wa habari utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara akimkabidhi
kombe nahodha wa timu ya Temeke mara baada ya kuibuka washindi wa
Mashindano ya Proin Women Taifa Cup ambayo yalichezwa katika Dimba la
Azam huku Proin Promotions na Azam wakidhamini mashindano hayo.
Nahodha
wa Timu ya Pwani akipokea Mfano wa hundi ya Shilingi Milioni Mbili
ambazo ni zawadi ya Mshindi wa pili katika Mashindano ya Proin Women
Taifa Cup na kuwamalizika kwa Temeke kuwa Mabingwa kwa kuifunga Pwani
goli 1 kwa 0.
Nahodha
wa Timu ya Ilala ambao ni washindi wa tatu akipokea mfano wa hundi
yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 ambayo mshindi wa tatu katika
Mashindano hayo ni Ilala
Waziri
wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (wa kwanza kulia)
na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi
wakishuhudia fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup mechi
iliyochezwa katika dimba la Azam Complex kwa kuzikutanisha timu za Pwani
na Temeke na Temeke Kuibuka Bingwa wa Proin Women Taifa Cup kwa
kuichapa Pwani goli 1 kwa 0.
Kikosi cha Timu ya Pwani
Kikosi
cha Timu ya Temeke ambacho kimeifunga Kikosi cha Timu ya Pwani kwa goli
1 kwa 0 katika Mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa
Cup, mchezo uliomalizika kwa Temeke kuibuka mabingwa wa Proin Women
Taifa Cup katika Dimba la Azam Complex
Waziri
Mukangala akisalimiana na timu ya Temeke pamoja na timu ya Pwani kabla
ya Mechi ya Fainali ya Proin Women Taifa Cup kuanza katika dimba la
Chamanzi Complex. Temeke iliibuka Mshindi kwa kuifunga Pwani Goli 1 kwa 0
No comments:
Post a Comment