Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliyemtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya kikazi ya siku nne kwenye kijiji cha Ololosokwani na halmashauri ya Ngorongoro kwa ajili ya maandalizi ya mradi wa kijiji cha digitali unaoendeshwa na Unesco kwa kushirikiana na Ki-elektronic ya Samsung unaotarajiwa kuwasili kijijini hapo mwezi februari ukitokea jijini Dar.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali (katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kulia) aliyeambatana na wataalamu wa elimu, afya na mawasiliano pamoja na Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya na ustawi wa jamii. Dkt Liggy Vumilia (hayupo pichani) . Kutoka kushoto wa kwanza ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias, Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wataalam wa Elimu, Afya, Utamaduni na Kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro jijini Arusha. Kushoto pichani ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter Kitenyi.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo na mkuu wa wilaya hiyo kabla ya kuelekea kijiji cha Ololosokwani kwa ajili ya mkutano na wanakijiji wa kijiji hicho kabla ya kuwasili kwa mradi wa kijiji cha kidigitali mapema mwezi februari.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akielezea changamoto za miundo mbinu ya barabara kwa kutumia picha alizopiga akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ololosokwan kupitia barabara ya Lake Natron kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akielezea jitihada zitakazofanywa na wilaya yake katika kuhakikisha miundo mbinu ya barabara inarekebishwa kuondoa usumbufu kwa magari mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali cha Ololosokwan yanapita bila kikwazo mapema mwezi februari.
Wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Unesco pamoja na Wizara ya afya wakitazama picha hizo kwenye kompyuta mpakato ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira
Rodrigues ameonesha mashaka yake juu ya ubora wa barabara ambazo magari
mazito yenye vifaa vya kijiji cha digitali Ololosokwan yanaweza kupita.
Alisema hayo kwenye mazungumzo na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Elias Wawa Lali wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Akiwa katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya kumwelezea shughuli
za Unesco katika wilaya yake, Mkurugenzi Mkazi huyo alipata nafasi ya
kuzungumzia haja ya kuboreshwa kwa maaneo kadha ya barabara kuelekea
kijiji cha Olosokwan ili kuyawezesha magari hayo makubwa kufika kwa
urahisi.
Huku akimuonesha mkuu wa wilaya baadhi ya picha alizopiga
akiwa njiani kukagua njia ya kupita magari hayo na kuangalia maandalizi
ya mwisho ya mradi huo mkubwa na wa kipekee nchini alisema hali ya
barabara si nzuri hata kidogo.
Vifaa kwa ajili ya kijiji hicho vipo bandarini tayari na
magari yanayoweza kubeba makontena hayo ni makubwa na barabara za
kuelekea kijiji hicho ni mbaya.
Kuwapo kwa kijiji hicho ni matokeo ya mkataba uliotiwa saini kati ya UNESCO na kampuni ya elektroniki ya Samsung mwaka jana.
Katika makubaliano hayo yalitiwa saini na Mwakilishi mkazi
Unesco nchini, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics
nchini Tanzania, Mike Seo katika Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye
Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na
kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu
(Telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji
hicho.
Mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu
kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa
wakipata shida ya kupata elimu.
Kupitia kijiji hicho vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao.
Wakati wa utiaji saini Mkurugenzi wa Samsung Electronics
nchini Tanzania alitaja miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana
katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ambayo ni pamoja
na kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.
Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika
uanzishaji wa vijiji vya digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika
inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta
mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
waliopo vijijini.
Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya
kidigitali barani Afrika.Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa
mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment