Na Faki Mjaka, Mascut Oman.
Maonesho ya Kimataifa ya
Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut nchini Oman yamechukua sura
mpya baada ya Nchi Washiriki kupeleka Wasanii wake wa Ngoma za Asili kwenda
kutumbwiza katika wiki mbili za mwisho ya Maonesho hayo. Tanzania ni moja ya nchi
washiriki ambapo Wasanii wake 15 Usiku wa jana walipata nafasi ya kuburudisha
kwenye Jukwaa kuu la Maonesho hayo.
Akizungumza kuhusu ujio
wao Kiongozi wa Wasanii hao wa Ngoma Bi Asha Khatib amesema wamejiandaa vizuri
kuhakikisha wanazikonga vyema nyoyo za Waomani kwa burudani ya nguvu. Amefafanua kuwa Waoman
wengi wanapenda Ngoma zenye asili ya Zanzibar hivyo wamefanya Mazoezi ya
kutosha ili kuwafurahisha Mashabiki wao pale wanapopanda Jukwaani kwa ajili ya
kutumbuiza.
“Kwa kweli tumejiandaa
vizuri tu na tumekuja hapa Mascut kwa kazi moja tu ya kutoa Burudani hivyo
Waoman wazidi kuja kwa wingi kuja kujionea burudani ya aina yake yenye Asili ya
Tanzania-Zanzibar”Alisema Bi Asha. Bi Asha amebainisha kuwa
katika Jukwaa watapiga baadhi ya Ngoma zenye Asili ya Zanzibar kama vile Msewe,
Uringe, Gonga, Kyaso,Kitua tua,Kibunguu na Kidumbaki ambapo anaamini zitakidhi
kiu ya burudani kwa Waomani.
Jana ikiwa ni siku ya
mwanzo kwa Watanzania hao hivyo walipewa muda wa nusu saa kwa ajili ya
kusalimia jukwaa na kutumbuiza ambapo walipiga Ngoma ya Msewe na Kitua tua.
Kabla ya Watanzania
kupanda Jukwaani kwenda kutumbuiza walitanguliwa na Wasanii kutoka Ufaransa
ambapo baada ya Watanzania kumaliza Wasanii kutoka Urusi ndio waliochukua
nafasi kutumbuiza. Nchi nyingine zilizopata
nafasi ya kutumbuiza katika Jukwaa kwenye Maonesho hayo ya Kimatifa ya Sanaa,
Ubunifu na Utamaduni ni pamoja na China, Iran, Thailand, India, Uzbekistani na
Misri.
Kwa wiki mbili mfululizo
kuanzia jana Wasanii wa Nchi hizo zinazoshoriki Maonesho ya Kimataifa ya
Sanaa,Ubunifu na Utamaduni watakuwa wakipanda katika Jukwaa kuonesha vipaji
vyao vya Muziki wa Asili ya nchi zao husika.
Wasanii hao wa Ngoma
waliofika Juzi kutoka Tanzania wanaungana na Wenzao waliokuwepo Oman kwa zaidi
ya wiki mbili sasa kushiriki Maonesho hayo ambapo Wasanii huonesha bidhaa zao
wanazozitengeneza kwa Mikono na kuwauzia Wateja mbalimbali wanaofika katika
Maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment