UONGOZI
wa Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) Kampasi ya Mbeya umewashukuru wananchi kwa
kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa mafanikio makubwa katika kipindi ambacho
wanasherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Chuo
hicho kinachomilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
Wizara ya Biashara na Viwanda kilifungua tawi lake Mkoani Mbeya mwaka 2013
hivyo kupata mwitikio mkubwa katika kipindi kifupi.
Akizungumza
na Mtandao wa Mbeya yetu blog, Mkuu wa Chuo hicho kampasi ya Mbeya, Dionise
Lwanga alisema wakati tawi la Mbeya linafunguliwa lilikuwa linatoa wanafunzi
katika ngazi ya Cheti lakini sasa kinatoa wahitimu wa Stashahada ya
kawaida(Diploma).
Lwanga
alisema Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamekipokea Chuo hicho vizuri pamoja na kutoa
ushirikiano mkubwa kwani hadi sasa wananchi wa Kata ya Iganzo jijini Mbeya
wamekipatia Chuo eneo la kujenga lenye ukubwa wa Heka 55.
Mkuu
huyo wa Chuo aliongeza kuqwa mbali na kupatiwa eneo la kujenga Chuo pia kuna
ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na Kampasi ya Mbeya ambapo katika mwaka
wa masomo wa 2013/2014 kulikuwa na wanafunzi 44 na mwaka 2014/2015 chuo kina
wanafunzi 165 kati yao 103 ngazi ya cheti na 62 wakichukua stashahada.
Alisema
katika mwaka wa masomo 2015/2016 Chuo hicho kinauwezo wa kuchukua wanafunzi 300
kutokana na kuendelea kuboresha mazingira na pamoja na upatikanaji wa nyumba za
kulala wanafunzi wanaotoka mbali(hostel) ambazo ziko karibu kabisa na Chuo.
Lwanga
alisema katika kusherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Chuo hicho
kimeanzisha utaratibu wa kuwafundisha watumishi wanaojiandaa kustaafu, kutoa
masomo ya ujasiliamali kwa wafanyabiashara na vikundi vinavyojihusisha na
ujasiliamali elimu ambayo hutolewa bure na uongozi wa Chuo unaweza kuwafuata
popote ingawa hutoa masomo katika muda wa jioni na muda wa kawaida(Full time).
Alisema
kwa mwaka wa masomo 2015/2016 Chuo kimeanza kutoa nafasi za kujinga ambapo
masomo yanatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu kwa wanafunzi wenye sifa
wanatakiwa kuwahi mapema.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment