Mkurugenzi
wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu akizungumza wakati wa
uzinduzi wa huduma za shirika hilo kupitia mkongo wa taifa wa
mawasiliano ambapo matawi yote nchini ya shirika hilo yameunganishwa
pamoja na makao makuu ili kurahisisha huduma za bima zinazotolewa na
Shirika hilo nchini kote, Amesema kwa sasa baada ya Kampuni ya simu ya
TTCL kufanya kazi nzuri ya kuunganisha mtandao wa huduma za NIC nchini
kote kupitia mkongo wa mawasiliano wa taifa mteja anaweza kuhudumiwa
mahali popote kama vile yuko makao makuu ya NIC Dar es salaam bila
kufuata huduma hiyo mbali. Hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya
NIC mtaa wa Samora jijini Dar es salaam leo, Katika picha kulia ni
Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura. Mkurugenzi
wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura akielezea kazi
nzuri iliyofanywa na shirika lake la TTCL katika kuunganisha matawi ya
NIC mikoani na Makao makuu ili kuleta pamoja huduma za bima zinazotolewa
na shirika hilo hapa nchini, Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima
la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu.
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu. akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi
wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura mara baada ya
kukamilisha kazi ya kuunganisha shirika hilo na mkongo wa mawasiliano wa
taifa. Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura na wa tatu kutoka kulia na Mkurugenzi
wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu wa pili kushoto
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
kutoka kushoto ni Meneja mradi Bw. Mihayo Ngawalina kutoka TTCL , Mtaalam wa Idara ya Teknohama NIC Bw. Sam Kamanga na kushoto ni Peter Ngota Afisa Mauzo na Masoko TTCL. Mtaalam wa Idara ya Teknohama NIC Bw. Sam Kamanga akizungumza na kuuelezea mradi huo wakati wa hafla hiyo kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu na Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura. Meneja mradi Bw. Mihayo Ngawalina akielezea jinsi mradi huo ulivyotekelezwa na faida zake kwa Shirika la Bima la Taifa NIC. Baadhi
ya maofisa na wakuu wa vitengo kutoka Shirika la Bima la Taifa NIC
wakifuatilia jambo wakati Meneja mradi wa TTCL alipokuwa aiuelezea. Kutoka
kulia ni Maofisa kutoka mashirika hayo Leonard Laibu Mkurugenzi wa
Huduma kwa wateja, TTCL,wa tatu Peter Ngota Afisa Masoko na Mauzo na
Sam Kamanga Mtaalam wa Teknohama NIC Leonard Laibu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja, TTCL kulia na baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari waliohudhuria katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment