Immaculate Makilika –MAELEZO ARUSHA
Rais wa
Shirikisho la Ujerumani amesema Serikali yake iko tayari kushirikiana
na Mahakama ya Afrika katika utendaji kazi wake ili kusaidia kutoa
huduma iliyokusudiwa kwa walengwa.
Rais huyo
ameyasema hayo leo alipotembelea Mahakama ya Afrika iliyopo mjini
Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku sita nchini na kusema
kuwa angependa kuona utawala wa sheria ambao unaozingatia demokrasia
unafuatwa na kuheshimiwa.
Aidha, Rais
Ghauck ameipongeza mahakama hiyo kwa weledi wake na hatua nzuri
waliyofikia huku akitolea mfano kesi iliyosikilizwa mwaka 2014 huko Adis
Ababa, Sudan.
‘Tunaunga mkono maendeleo pia tungependa kuendelea kushirikiana nanyi, msisite kutuomba msaada alisema Rais Gauck’.
Naye kwa
upande wake Jaji Mkuu wa Mahakama ya Afrika Augustino Ramadhani alisema
Serikali ya Ujerumani imekua na ushirikaiano mzuri na Mahakama hiyo
kwani ilisaidia pia katika ujenzi wake.
Hata hivyo
jaji Ramadhani amesema wamemuomba Rais wa Ujerumani asaidie kujenga
mahakama ya Afrika ya Mashariki, ombi ambalo Rais huyo amesema
atalishughulikia kushirikiana na viongozi aliongozana nao.
Aidha, Jaji
Ramadhani amesema kuwa uwepo wa Mahakama hii Afrika ni jambo la
kujivunia kwani itaweza kusaidia matatizo ya waafrika wote kutoka
sehemu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment