TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 5, 2015

Serikali yatenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kukuza ajira

anne
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela
…………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-Maelezo ,Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya kazi na Ajira imetenga kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kukuza ajira kwa vijana.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Susan Lyimo kuhusu mkakati wa serikali kuwakopesha vifaa wahitimu wa mafunzo ya Veta ili kujiajiri.

Aidha aliongeza kuwa kupitia mpango huo, Serikali ina lengo la kuwapatia vijana mitaji yenye masharti nafuu na nyenzo za uzalishaji mali ili waweze kujikimu kimaisha na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
“Ili kufanikisha hili nawaomba vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi waweze kujiunga katika vikundi kwa kuandika mpango mradi kwa ajili ya kuomba mkopo ili kupata mitaji na vitendea kazi” alisema Kilango
Aliongeza kwamba Halmashauri za wilaya, Miji na Majiji zimekuwa zikitenga asilimia 5 ya bajeti zake kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata mikopo wakiwemo wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi kutoka vyuo vya VETA.
Vilevile alieleza kuwa ili kuhakikisha vijana wanaohitimu vyuo vya ufundi stadi wanaweze kujiajiri mada zinazohusu Taasisi za Fedha pamoja na somo la ujasiriamali zimekuwa zikitolewa ili kuwawezesha kujiajiri na kupata mikopo.

No comments:

Post a Comment