…………………………………………………………………………………………
Pamoja
na kuwepo kwa changamoto za kushuka kwa bei ya mafuta duniani, Tanzania
bado imeendelea kuvutia wawekezaji kutoka pande zote za Dunia kuja
kuwekeza katika shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini. Akiongea
katika mkutano wa mwaka wa GE Oil & Gas, Waziri wa Nishati na
Madini Mhe. George Simbachawene (MB) aliwaalika wawekezaji wakubwa
kutoka pande zote za dunia kutembelea Tanzania na kuona nafasi za
uwekezaji zilizopo.
Mkutano
huo uliofanyika Florence, Italy uliwakutanisha wadau wakubwa wa Mafuta
na Gesi duniani kujadili changamoto katika sekta hiyo na namna ya
kuzikabili. Kauli mbiu ya mwaka huu ililienga zaidi kuangalia namna
ambavyo sekta hii itachochea maendeleo ya dunia nzima kwa kuhakikisha
kuwapo kwa nishati endelevu na yenye kujali mazingira. Tanzania
iliwakilishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dr. James Matargio
ambaye alipata fursa ya kuitangaza Tanzania kwa kuonyesha fursa zilizopo
katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini. Dr. Mataragio alisema “ pamoja
na kuwa bei za mafuta zinaendelea kushuka, bado kuna fursa ya kutumia
gesi kusaidia upatikanaji wa nishati endelevu na yenye kulinda mazingira
kwa vizazi vya sasa na baadae”
No comments:
Post a Comment