Nyota na msanii mkongwe wa muziki wa bongo flava nchini
Tanzania, Juma Nature amesema kuwa wasanii wakongwe wa muziki huo
watapotea kabisa katika ramani ya muziki kama wadau wa muziki pamoja na
vyombo vya habari havitawapa nafasi ya kutosha kama wanavyopewa wasanii
wengine wa sasa.
Nature amesema kuwa zamani kipindi yeye yupo Bongo Records wasanii
wote walikuwa kitu kimoja na kazi zao walikuwa wanafanya kwa
kushirikiana na kwa umoja kitu ambacho kilifanya wote kuwa na mafanikio
sawa kwani hata maonesho yao walikuwa wanagawana fedha sawa kitu
kisichowezekana kwa sasa.
Nature amesema kuwa kwa sasa wasanii kama yeye watapotea kutokana na
wadau wa muziki kuwatumia wasanii wachache katika shughuri zao za kila
siku huku akitolea mfano jinsi Diamond anavyopewa kipaumbele katika
maonesho na kazi nyingine huku wasanii wazuri kama Rich Mavoko na Ali
Kiba wakisahaulika kitu kinachosababisha kuwa na matabaka kwani
wanaopewa nafasi ndio wanaofanikiwa.
Katika hatua nyingine Juma Nature amewaasa wadau wa muziki
kutowasahau wakongwe wa muziki nchini kwani wao ndio walioufikisha
muziki huu hapa ulipofika.
No comments:
Post a Comment