Meneja Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na
wanahabari (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa
king’amuziki kipya cha DStv HD leo jijini Dar. Kulia ni kwake
ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na
kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.
Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania
wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya
cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.
Akizungumza na wandishi wa habari
mapema leo jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice
Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema
king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye
ubora mzuri zaidi.
Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.
“Wateja wa DStv watafurahia
ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati wa
kuchangamkia ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania”
alisema Ronald Shelukindo.
Meneja uendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king’amuzi
hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo
jijini Dar.
Ronald Shelukindo akielezea kwa
kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali
ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame
kipi gani, muda gani na wakati gani?.
King’amuzi cha “DStv HD, mteja
anaweza kujipangia atazame kipindi gani ama kwa wakati autakao yeye,
ambapo anachoweza ni kuseti hicho kipindi akipendacho na kisha anaweza
kukiangalia kwa wakati wake, hata kama muda umepita kwa wakati huo
kinarushwa kwenye chaneli husika” alifafanua Ronald Shelukindo.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa
MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu aliwahimiza watanzania
kuchangamkia vinga’muzi hivyo vya DStv HD, ambavyo kwa sasa vipo karibu
maduka yote ya Mawakala wa DStv, kwa bei rahisi kabisa vikiwa
vinapatikana kwa sh 99,000/ kwa mteja mpya huku kwa wateja walio na
ving’amuzi vya zamani vya DStv watakaotaka kubadilishiwa, watalipia sh
39,000/ tu.
Meneja uendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha king’amuzi kipya cha
DStv HD kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
“Ofa hii ni kwa ajili ya kipindi
hiki cha fainali za AFCON, hadi hapo michuano hii itakapofikia tamati
ambapo bei itabadilika kutoka hizi za sasa, hivyo ni wakati wa
kuchangamkia ofa hii ya kipekee na kwa mara ya kwanza, kupata kitu cha
ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi.” Alisema Furaha Samalu.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa
MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi alieleza kuwa, siku zote
MultiChoice itaendelea kuwa mstari wa mbele kwa kutoa huduma zilizo bora
na za kisasa katika ulimwengu huu wa digitali ambapo bidhaa hizo za
DStv zimeendelea kuwa bora kila siku.
“Huduma za DStv siku zote
zimekuwa bora ikiwemo kutoa huduma zisizoleta usumbufu. Ving’amuzi
vyetu daima vinaonyesha ubora wa hali ya juu na hutoweza kusumbuliwa na
ukatikaji wa picha ama mikwaruzo… Hivyo ni wakati sasa wa kuchangamkia
ofa hizi.” Alibainisha Barbara Kambogi.
Meneja Masoko wa Multichoice
Tanzania, Furaha Samalu akifafanua bei za king’amuzi hicho kipya ambapo
kwa wateja wapya watajipatia kwa ofa ya Tsh. 99,000/ kuanzia leo hadi
siku Jumapili kilele cha fainali za michuano ya AFCON huku ambao ni
wateja tayari wanabadilishiwa kwa gharama ya Tshs. 39,000/ ambayo pia
ni ofa. Ving’amuzi hivyo vipya vya DStv HD vinapatikana kupitia mawakala
wote wa DStv Tanzania nzima.
Katika hatua nyingine, DStv
wamezindua huduma mpya kwa wateja wao waliounganishwa na ving’amuzi
hivyo vya DStv kuweza kuendelea kufurahia huduma hiyo kupitia simu zao
za viganjani zenye uwezo wa ‘Android’, Kompyuta mpakato (Laptop),
Tablet, na vifaa vingine vyenye uwezo wa kupokea usajili wa ‘App’.
Akielezea, juu ya huduma hiyo,
Ronald Shelukindo, alibainisha kuwa, kinachotakiwa ni kwa mteja wa DStv,
kwenda kwenye simu yake au Laptop, ama Tablet na kisha kujisajili
kupitia ‘App’ kwa kujisajili kwa kuandika ‘DStv Now’.
Aidha, Ronald Shelukindo
alisisitiza kuwa, huduma hiyo ya DStv Now ni kwa wateja waliouganishwa
na ving’amuzi hivyo tu ambapo wataifurahia huduma hiyo kwa kuendelea
kuangalia chaneli zaidi ya 12 za DStv, ikiwemo ya Super Sport 3, za
filamu, na nyinginezo mbalimbali.
Pia kwa maelezo zaidi wateja wanaweza kutembelea tovuti ya DStv.com
Meneja uendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionesha huduma mpya ya DStv
Now ambayo mteja ataweza kuangalia vipindi vya DStv kupitia simu yake ya
kiganjani, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na Tablet. Huduma hii ni
kwa wateja ambao wameunganishwa na ving’amuzi vya DStv kupitia akaunti
zao.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice
Tanzania, Barbara Kambogi (katikati), Meneja uendeshaji wa Multichoice
Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Meneja Masoko wa Multichoice
Tanzania, Furaha Samalu (kushoto) wakiangalia promo ya namna ya kujiunga
na huduma ya DStv Now “application” inayopatikana katika simu zote za
Android pamoja na kompyuta mpakato (Laptop) unajiunga kwa kutembelea www.dstv.com
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar leo.
Meneja uendeshaji wa
Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) na Meneja Masoko wa
Multichoice Tanzania, Furaha Samalu (kulia) na Meneja Uhusiano wa
MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (kushoto) wakipozi na king’amuzi
kipya cha DStv HD.
No comments:
Post a Comment