Wananchi
wakiangalia jengo la ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la
Lumumba, ambapo kilizaliwa chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi
wa jengo jipya la chama hicho Dar es Salaam jana
…………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
JENGO la
ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar es
Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili kupisha
ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye
alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.
“Tunachokifanya
katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida,”alisema Nape wakati
akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia tingatinga.
Kutokana
na kubolewa kwa jengo hilo , viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Katibu
Mkuu wa CCM,Abdulrhaman Kinana , watakuwa katika Jengo la Umoja wa
Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati ukarabati wa jengo
hilo lililobomolewa ukiendelea.
Awali
baadhi ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai kuwa jengo
hilo la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa ambalo
litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.
Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.
No comments:
Post a Comment