Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akimlaki na kisha kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam jana, Jumatano, Februari 4, 2015. PICHA NA IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif na ujumbe wake baada ya kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jana, Jumatano, Februari 4, 2015. PICHA NA IKULU

………………………………………………………………………………………………..
Tanzania imesema kuwa dhamira yake
ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na
itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi
inavyoruhusu.
Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran
katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili
hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka
maendeleo ya watu bila usumbufu na matishio ya ugaidi.
Mambo hayo mawili yamejadiliwa leo, Jumatano, Februari 4, 2015
katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya
Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif.
Mheshimiwa Zarif amewasili nchini leo akitokea Burundi katika
ziara ambayo pia imemfikisha Kenya, Uganda na Rwanda akifuatana na
maofisa wa Serikali na kundi kubwa la wafanyabiashara wa Iran.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais
Kikwete amemwambia Mheshimiwa Zarif kuwa Tanzania bado inakusudia
kufungua ubalozi mjini Teheran, mji mkuu wa Iran, kama ilivyoahidi na
kuwa itafanya hivyo hali ya kifedha na kiuchumi itakaporuhusu. Rais
ametoa maelezo hayo kufuatia ombi la Waziri Zarif kukumbushia umuhimu wa
kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania katika Iran.
“Tunakusudia kufungua balozi katika nchi marafiki ambako kwa
sasa hakuna balozi ikiwamo Jamhuri ya Kiislam ya Iran. Katika Afrika,
kwa mfano, tunapanga kufungua balozi katika Namibia, Angola, Algeria na
Ghana. Hizi ni nchi rafiki ambazo baadhi yake zimekuwa na balozi katika
Tanzania tokea uhuru wetu. Mbali na Iran katika Asia, tunaangalia nchi
kama Uturuki, Qatar na Kuwait na nyingine marafiki,” Rais Kikwete
amemwambia Mheshimiwa Zarif.
Kuhusu mapambano dhidi ya magaidi, Rais Kikwete amesema kuwa ni
muhimu kwa Tanzania na Iran kuwa na msimamo ulio sawa wa jinsi ya
kukabiliana na ugaidi.
“Wakati wote, sote tunakabiliwa na matishio ya ugaidi na hivyo
tunalazimika wakati wote kuwa macho na uwezekano wa mashambulizi ya
kigaidi. Sisi Tanzania bado tunakumbuka shambulio dhidi ya Ubalozi wa
Marekani hapa nchini. Ulishambuliwa Ubalozi wa Marekani lakini watu wote
waliopoteza maisha yao ni Watanzania.”
Rais Kikwete na Mheshimiwa Zarif pia wamejadili jinsi gani
Tanzania na Iran zinavyoweza kuongeza ushirikiano wa kibiashara na
uwekezaji katika maeneo mbali mbali ya uchumi na Rais Kikwete amemweleza
Waziri fursa zilizoko katika sekta za nishati na reli.
Waziri Zarif pia amemkumbusha Rais Kikwete mwaliko wa kumwomba Rais Kikwete kutembelea Iran kwa ziara ya Kiserikali.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,DAR ES SALAAM.
4 Februari, 2015
No comments:
Post a Comment