Mkuu
wa matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Mayengoh, akikabidhi vitabu
kwa mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kwenye wodi maalum ya watoto wanaougua ugonjwa wa saratani katika
kuadhimisha siku ya saratani duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya
wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi wa watoto hao. Benki hiyo
ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula, vifaa vya kuchezea,
sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusiana na
ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku
ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la saratani “lipo ndani ya
uwezo wetu”.
Meneja
masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono
na Dr. Livin Mumbari Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa
watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto
wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani
duniani. Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi
wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula,
vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga
uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu
ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la
saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
No comments:
Post a Comment