Waziri wa Ujenzi Dkt. John
Pombe Magufuli amewahakikishia wakazi wa mji wa Tunduma mkoani Mbeya kuwa Serikali
itajenga barabara ya njia nne katika mji huo ili kupunguza msongamano wa magari
na kuuwezesha mji huo kuwa wa kisasa na kibiashara.
Amesema hayo katika ziara
yake ya ukaguzi wa miradi ya barabara inayoendelea katika mikoa ya Mbeya na
Rukwa ambapo akiwa mjini Tunduma amekutana na wananchi wanaofanyabiashara
katika mji huo.
“Dumisheni umoja,amani na
mshikamano ili mfanye biashara zenu na kukuza uchumi nasi tutahakikisha
tunajenga barabara ya njia nne ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha
mji wa Tunduma kuwa wa kisasa na kibiashara na hivyo kuwa mahali pazuri pa watu
kuishi”,amefafanua waziri Magufuli.
Katika ziara hiyo waziri Magufuli
amekagua mizani ya Nkangamo na barabara ya Tunduma –Sumbawanga KM 225, iliyojengwa
kwa kiwango cha lami na kuwataka wananchi wa mkoa wa Rukwa kutumia barabara hiyo
kukuza uchumi wao na wa mkoa wao kwa kufanyakazi kwa bidii.
Akihutunbia wananchi wa
Sumbawanga Waziri Dkt. Magufuli amewataka wananchi kutambua kuwa barabara za
lami zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo wazitumie kwa manufaa na wale walioko
kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao mapema ili kuwezesha ujenzi
kufanyika kwa wakati.
Waziri Magufuli amesema Serikali
iko katika hatua za awali kujenga barabara ya Matai-Kasesha KM 50 kwa kiwango
cha lami ili kuunganisha mkoa wa Rukwa nan chi ya Zambia na hivyo kuvutia
wawekezaji wengi kuwekeza mjini Sumbawanga na hivyo kutoa fursa za ajira na
uchumi kwa wananchi.
Waziri Magufuli yuko
katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya barabara katika mikoa ya Mbeya,Rukwa,Katavi
na Tabora ambako kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami
inayoendelea.
Imetayarishwa
na kitSengo cha habari na mawasiliano serikalini wizara ya ujenzi.
No comments:
Post a Comment