Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela akijibu swali la Mh. Joseph Selasini Mbunge wa Rombo.
Mbunge la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, akiuliza swali.
………………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela
ametoa wito kwa wamiliki wote wa shule binafsi pamoja na za serikali
kuzingatia kiwango cha ufaulu kutoka kidato kimoja kwenda kingine
kilichowekwa na serikali.
Akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, bungeni mjini
Dodoma aliyetaka kujua kama Serikali inajua na kuunga mkono kiwango cha
ufaulu kwa shule zisizo za Serikali zinazoweka viwango maalum vya
ufaulu tofauti na vile ilivyoviweka.
Naibu Waziri Anne Kilango alisenma Serikali haiungi mkono
utaratibu huo kwa kuwa umekiuka waraka wa elimu namba 12 wa mwaka 2011
na waraka Namba 4 wa mwaka 2012.
“Napenda kusisitiza kuwa yeyote atakayekaidi maelekezo haya ya
serikali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa sheria ya
elimu Namba 25 sura ya 353 kifungu cha 35” alisema Kilango
Aliongeza kuwa Waraka wa Elimu Na. 6 wa mwaka 2011 umetoa
maelekezo kuhusu wastani wa ufaulu katika mtihani wa Kitaifa wa kidato
cha pili ambao ni asilimia 30.
Hivyo aliwataka walimu waelewe kuwa wanafunzi wanatofautiana
katika uelewa hivyo kuweka kiwango kikubwa cha wastani kunasababisha
wanafunzi kukosa fursa ya kuendelea na masoma na hivyo kuanza utaratibu
mpya ya kutafuta shule.
Alibainisha kuwa Serikali itazindua program ya KKK Februari 7,
2015 ikiwa na nia madhubuti ya kuboresha elimu kwa shule zote za
serikali katika kutoa elimu bora kwa wananchi .
No comments:
Post a Comment