Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akihutubia katika
maadhimisho ya siku ya sheria nchini Mkoni Rukwa leo tarehe 04/02/2015
katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga. Kaulimbiu ya
maaadhimisho hayo ikiwa “Fursa ya kupata haki: Wajibu wa Serikali,
Mahakama na Wadau”. Katika hotuba yake hiyo alisema ipo haja kubwa kwa
Serikali kubadili sheria zake ili lugha ya mahakamani na hukumu
ziandikwe kwa kiswahili. Kwa upande wa wananchi aliwaasa kujiepusha na
tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kudumisha amani nchini.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo akipokea
gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha Jeshi la Polisi wakati wa
maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoani Rukwa leo tarehe 04/02/2015.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo katikati
akisoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya sheria Mkoani Rukwa ambapo
aliwataka mahakimu wote Mkoani Rukwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa
mujibu miongozo ya mahakama ili kusaidia uharakishwaji wa utoaji haki
kwa wananchi kwa wakati. Aliwaeleza pia wadau wote wa sheria wakiwepo
mawakili wa kujitegemea kuwa mashauri yote ya kesi yatakua yakisimamiwa
na kutolewa maamuzi na mahakama na sio mawakili kutaka kuingilia
utendaji wa mahakama.
Baadhi ya wadau na viongozi wa Sheria na Serikali katika meza kuu.
Sehemu ya mahakimu, mawakili, wanasheria na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment