Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) na mgeni wake Rais wa Shirikisho la
Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakifurahia wakati wa dhifa ya kitaifa ya
chakula cha usiku aliyomwandalia
kiongozi huyo jana usiku, Ikulu
jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa
Shirikisho la
Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakiwa wamesimama wakati
wimbo taifa wa Tanzania na ujerumani ulipopigwa wakati wa dhifa ya
kitaifa ya
chakula cha usiku aliyomwandalia
kiongozi huyo jana usiku, Ikulu
jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na
Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Askofu Gehazi Malasusa (wa pili kutoka kushoto) na viongozi wengine wa Serikali
wakiwa kwenye dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyoandaliwa Rais wa
Ujerumani Joachim Schadt na Rais Jakaya Kikwete jana usiku jijini Dar es
salaam.
Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni
wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakielekea sehemu ya nyuma
ya ukumbi kutazama Brass bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitoa burudani
wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomuandalia mgeni wake jana
usiku Ikulu jijini Dar es salaam.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto)
akiongea na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania Diana Melrose (aliyesimama) wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha
usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya
Kikwete kwa Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck , Ikulu jana usiku.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck
akitoa ujumbe wake kwa wageni mbalimbali waliohudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa
na Rais Jakaya Kikwete Ikulu.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck
na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama Brass Bendi ya Jeshi la Polisi
iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama vikundi mbalimbali vya ngoma za asili
vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete akizungumza jambo na Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na mkewe Bi.Daniella
Schadt wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyowaandalia wageni
hao jana Usiku, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck
(wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan
Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella
Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi.
No comments:
Post a Comment