Ma
Dj wakitoa burudani wakati wa kusherekea miaka mitano ya Grooveback Djs
ambayo inaundwa na Ma Dj maarufu nchini, Dj Peter Moe, PQ, Crucial,
KT, Tony na JB, iliyofanyika katika bar maharufu ya East 24 iliyoko
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Ma Dj
waalikwa wa kimataifa waliokuwepo ni Dj Pinye na Dj Nijo kutoka Kenya.
Grooveback wanapiga Disco la nguvu kila jumamosi East 24 Bar, Arcade
House, chini ya udhamini wa Windhoek Lager – 100% PURE BEER.Mashabiki mbalimbali wakipata burudani wakati wa Kusherekea miaka mitano ya Grooveback Dj
Mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo, Jerome Rugemarila (katikati), akiwa na warembo wa kampuni hiyo.
Wana habari Dotto Mwaibale (kushoto), Faustine Kapama (katikati), wakiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Mabibo, Boniface.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika hafla hiyo, Ofisa Mauzo wa Kampuni ya
Mabibo, Kelvin Coster alisema muitikio wa wapenzi wa muziki ulikuwa ni
mkubwa.
“Mashabiki ni wengi mno waliofika kushiriki sherehe hii ya kutimiza miaka mitano ya upigaji muziki wa disco” alisema Coster.
Alisema
kampuni hiyo iliamua kudhamini sherehe hiyo kupitia kinywaji cha
Windhoek kinachopendwa na watu wengi kutokana na ubora wa kimataifa na
bei yake kuwa nafuu.
”
Napenda kusisitita kuwa Windhoek ni bia ambayo ukinywa haileti matatizo
yoyote kama ya kuumwa kichwa, mnywaji akiamka asubuhi atajisikia vizuri
pasipo mzingio wa ziada” alisema Coster.
Alisema
wanywaji wanapaswa kuzingatia kunywa bia yenye namba MB66 ambayo
inauzwa kwa chupa sh.3,000 na katoni kwa sh.58,000 ambapo faida yake ni
sh.14,000 na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment