Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa na watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga wilaya ya Iringa jimbo la kalenga ambako alifika kukabidhi msaada wa chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya mwaka mpya kwa watoto hao |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa karibu na gari lililobeba msaada wa chakula |
Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga Iringa wakiwa wamepumzika |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akiwa amemshika mmoja kati ya watoto yatima kituo cha Tosamaganga kushoto ni diwani wa viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra Kiwanga ambae alikuwa ni mwenyeji wa Mungai katika kukabidhi msaada wa chakula kwa yatima hao |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai akiwa na mmoja kati ya watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga Iringa leo |
Mlezi wa watoto hayo Sisita Herena Kihwele kushoto akiwa na ugeni uliofika kituoni Tosamaganga kwa ajili ya kushuhudia tukio la Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kukabidhi msaada wa chakula xcha mwaka mpya kwa watoto kituoni hapo |
Watoto hao yatima wakiimmba mbele ya ugeni |
Mtoto aliyefahamika kwa jina la Nyota akimsalimia Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai ambae alifika kituoni hapo leo kuwapa watoto hao chakula cha sikukuu ya mwaka mpya ,mtoto huyo alitelekezwa porini na mzazi wake baada ya kujifungua kabla ya kituo hicho kumuokota na kumtunza kituoni hapo |
Baadhi ya yatima kituo cha Tosamaganga |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia akiwa na mlezi wa kituo hicho sisita Herena Kihwele |
Watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga wakimpongeza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kwa kuwajali kwa mwaka mpya |
Diwani wa viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra Kiwanga kushoto akimpongeza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa Ya GNSM Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai kulia kwa kusaidia yatima |
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa ya GNSM
Contractrors Co. Ltd Bw Geofrey Mungai amekabidhi msaada wa chakula
cha mwaka mpya chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 1.5 kwa
kituo cha kulelea watoto yatima cha Tosamaganga katika jimbo la
kalenga wilaya ya Iringa vijijini .
Akikabidhi
msaada huo leo Mungai alisema kuwa amelazimika kufika katika
kituo hicho ambacho kinasimamiwa na masisita wa kanisa la RC kama
sehemu ya mwendelezo wa kampuni yake kuendelea kuzungukia vituo
mbali mbali vya kulea yatima na kuwapa faraja hasa katika msimu huu
wa sikikuu.
Alisema
kuwa miongoni mwa vituo ambavyo amepata kuvikumbuka katika msimu huu
wa sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya ni pamoja na kituo cha Daily Bread
Life (DBL) kilichopo jimbo la Iringa mjini na kituo hicho cha
Tosamaganga kilichopo jimbo la Kalenga huku lengo likiwa ni
kuwakumbuka yatima hao na kuihamasisha jamii kuelekeza nguvu zao
kwa yatima kama hao.
Bw
Mungai alisema kuwa takwimu za maambukizi ya VVU katika mkoa wa
Iringa zimeendelea kuongezeka na iwapo jamii haitajenga utamaduni wa
kujali yatima vifo vya watoto yatima ambao watakosa chakula baada ya
kupoteza wazazi wao kwa VVU pia vitazidi kuongezeka hivyo lazima
misingi ya kuwajali yatima ikaanzwa kuwekwa mapema zaidi.
”
Hawa watoto iwapo jitihada za vituo vya kusaidia yatima visinge kuwa
na moyo huo leo yawezekana baadhi yao wasingekuwepo hapo tungekuwa
tumewazika ila kazi nzuri ya kujitolea inayofanywa na vituo vya
yatima ndio imewafikisha hapa leo ….hivyo lazima sisi kama jamii
kuunganisha nguvu zetu na vituo vya yatima”
Pia
alisema kuwa hata viongozi wa vyama vya siasa na serikali ni vema
wakaweka utaratibu wa kufanya ziara za mara kwa mara katika vituo
vya yatima na kujifunza mazingira ambayo watoto hao wanaishi ikiwa
ni pamoja na kusaidia kutatua changamoto zinazovikabili vituo vya
yatima mkoani Iringa .
Kwani
alisema kwa upande wake kama mkandarasi ambae amekuwa akifanya kazi
ya ujenzi wa barabara mkoani Iringa na nje ya mkoa ameona ni vema
katika fedha kiasi ambazo anazipata kuweka utaratibu wa kusaidia
watoto yatima kama njia ya kuwahamasisha pia wenzake kujitoa kwa
yatima katika maeneo yao ama kusaidia kuchangia maendeleo ya maeneo
yao.
Katika
hatua nyingine Mungai aliwapongeza walezi wa vituo vya yatima
katika mkoa wa Iringa kuwa kutokana na mchango wao wa kulea yatima
hata idadi ya yatima na watoto wa mitaani katika mji wa Iringa
imeonekana kupungua zaidi
Kwa
upande wake diwani wa viti maalum tarafa ya Kalenga Shakra
Kiwanga akimpongeza Mungai alisema kuwa ameonyesha upendo mkubwa
kwa yatima hao na kuwataka makandarasi wengine kuiga mfano huo.
Kiwanga
ambae pia ni mmoja kati ya makandarasi wadogo mkoani Iringa alisema
kuwa alichofanya Mungai ni somo kwao pia katika kutoa sehemu ya
makusanyo wanayoyapata kupitia kazi mbali mbali.
Awali
mlezi wa kituo hicho Herena Kihwele alisema kuwa kituo hicho kina
watoto zaidi ya 100 na kuwa kwa sasa kituo kinakabiliwa na changamoto
kubwa ya kushindwa kuwalipia ada sekondari watoto zaidi ya 10
waliofaulu darasa la saba ila kituo hakina uwezo wa kuwasomesha .
Iwapo
umeguswa kuchangia kituo hicho ada ama msaada wowote ule waweza
kuwasiliana na mlezi wa kituo hicho Sisita Herena Kihwele kwa simu
0768831477 pia waweza kutumia namba hiyo kwa kutuma M-PESA.
No comments:
Post a Comment