
NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
ALIYEKUWA
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Jeremiah Sumari amezikwa jana
kijijini kwake Akheri wilayani Meru Mkoani hapa na mazishi hayo
kuongozwa na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya
kikwete, pamoja na waziri mkuu Bw Mizengo Pinda.
Akiongea
na waombolezaji waliofika katika eneo hilo la Akheri waziri Pinda
alisema kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanatakiwa kuwa mfano wa
kuigwa kama alivyokuwa Bw Sumari
Bw
Pinda alieleza kuwa kiongozi kama kiongozi anatakiwa kuwa na sifa
ambazo zitamfanya jamii imlkumbuke mara zote na sifa hizo zinatakiwa
kuwa ni miongoni mwa sifa nzuri na zenye kulijenga taifa.
“hii ni safari ya Bw
Sumari lakini sote tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaweka hazina hapa
duniani, na kuwa na sifa nzuri na zenye kupendeza, kwa kuwa kifo ni
msingi wa kila mwanadamu hapa duniani”aliongeza bw Pinda.
Pia
aliitaka familia ya Marehemu Sumari kuhakikisha kuwa haioni mzigo kwa
kuondokewa na Baba yao na badala yake wahakikishe kuwa wanaendelea
kumtegemea zaidi Mungu katika mambo yao ikiwa ni pamoja na kufuata Mambo
mazuri ambayo yalikuwa yanafutwa na Bw Sumari.
Katika
hatua nyingine viongozi mbalimbali ambao waliongoza ibada hiyo ya
Mazishi walisema kuwa kwa sasa jimbo la Arumeru Mashariki limepoteza
Mbunge wake kwa maana hiyo ni lazima taratibu za kumtafuta Mbunge huyo
zifanyike wakati utakapofika lakini wagombe wanatakiwa kuwa makini na
kuachana na tabia ya uchakachuaji wa matokeo
Walibanisha
kuwa endapo kama zoedzi la uchakachuaji wa matokeo katika jimbo hilo ni
wazi kuwa watakuwa wanaweka jimbo hilo mashakani kabisa hali ambayo
itachangia matatizo mbalimbali juu ya jimbo hilo.
“tunatangaza
rasmi kabisa kuwa hapa hamna masuala ya kuachakachua matokeo kwa maana
hiyo uchaguzi utakaokuja ni lazima matokeo yawe ya halali kwa maslahi ya
jimbo hili”waliongeza wachungaji hao.
Aidha nao viongozi
wa chama cha mapinduzi (CCM) walisema kuwa wao kama chama kupitia kwa
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo walikuwa na ahadi nyingi dhidi ya jimbo
hilo ambapo ahadi hizo zilikuwa na lengo la kusaidia jamii.
Walisema kuwa ahadi za mbunge huyo kwa jimbo hilo ziko palepale na zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya chama hicho kwa eneo hilo la Arumeru Mashariki ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbali.
Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wameahidi kuendelea kushirikiana
na Wadau wa vyombo vya Habari hapa nchini kwa kutoa taarifa sahihi na
kwa wakati muafaka ili kuwawezesha wananchi kupata haki yao ya kikatiba
ya kupashwa habari.
Afisa
Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema
kuwa ahadi hiyo imetolewa na Makamanda wa Polisi kutoka mikoa mitatu ya
Unguja waliokuwa wakishiriki katika Mafunzo ya Uhusiano wa Polisi na
Vyombo vya Habari yaliyokuwa yakifanyika kwenye chuo cha Polisi
Zanzibar.
Akizungumza
kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja, ACP Aziz juma Mohammed, amesema Polisi na
Wanahabari ni watu wanaotegemeana kitaaluma na kwamba kazi ya Polisi
isingetambulika kwa urahisi kwa raia kama sio juhudi za vyombo vya
Habari.
Kamanda
Azizi amesema ili kuwawezesha Waandishi wa Habari kutangasa habari kwa
usahihi ni lazima Polisi nao wasiwe na kigugumizi katika kutoa taarifa
zinazohitajika kwa waandishi.
Amesema
kutoa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka, kunaondoa uvumi ama
minong’ono ya taarifa za kweli zilizokosa ufafanuzi kutoka kwa msemaji
wa eneo husika.
Naye
Kamaba wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja ACP Augost Uromi, ameitaja
mifano michache ya jinsi Polisi wanavyowahitaji Waandishi wa Habari kuwa
ni pamoja na kusaidia kueneza mpango wa Polisi Jamii na Ulinzi
Shirikishi jambo ambalo lingewawia Polisi vigumu kumfikia mwananchi moja
mmoja kumjulisha juu ya dhana hiyo.
Amesema
Vyombo vya Habari vinapotumika vizuri, huwawezesha watu wengi kupata
habari moja na kwa wakati mmoja na hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa Polisi
kuendelea kushirikiana kwa dhati na vyombo vya Habari na kuwaona ni
wadau muhimu.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja ACP Ahmada
Abdallah, amesema kuwa ili kuepuka waandishi kuandika taarifa zisizo
sahihi ni vema kila Kamanda kuwa tayari kutoa taarifa za matukio kila
yanapotokea.
Akitoa
mada wakati wa mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar SSP
Ramadhan Mungi, aliwaambia walishiriki wa hao kuwa ili kuepuka
upotoshwaji wa taarifa ni muhimu kila taarifa inayotolewa kwa waandishi
wa Habari iwe ya maandishi.
Awali akifungua Mafunzo hayo, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa Mafunzo
hayo yameandaliwa ili kuwawezesha Maafisa wa Polisi kujua namna ya
utayarishaji na usambazaji wa taarifa kwa vyombo vya Habari (Press
Release) na jinsi ya kuandaa na kufanya mikutano ya moja kwa moja na
waandishi wa habari. (Press Conference).
Mafunzo
hayo ya siku mbili ambayo yalikuwa yakifanyika kwenye Chuo cha Polisi
Zanzibar, (Zanzibar Police Academy) yamewashirikisha Kamakanda wa
Polisi wa mikoa yote ya Unguja, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhim
kutoka Mikoa ya Mjini Magharibi, Kusini na Kaskazini Unguja pamoja na
Maafisa Waandamizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
Zanzibar.








Benjamin Sawe
Maelezo
Dar es Salaam
Wasanii
wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wameshauriwa kuzisoma nyaraka
mbalimbali za Bodi ya Filamu ili wajue sheria na kanuni zinazohusu
tasnia ya hiyo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini Joyce Fissoo alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya Sheria namba 4 ya
Utengenezaji wa Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976.
Akifafanua
juu ya sheria hiyo, Bi Fissoo alisema ndiyo inayoendelea kutumika mpaka
sasa na kukanusha tuhuma zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari
kuwa ya uwepo wa matumizi ya sheria mpya.
“Hakuna
Sheria mpya ya Filamu na Michezo ya Kuigiza iliyotungwa, Sheria
inayoendelea kutumika ni ile ya mwaka 1976 bali kilichofanyika ni
utekelezaji wa kanuni za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ambapo
mchakato wake ulianza mwaka 2011.
Akizungumzia juu ya malalamiko ya baadhi ya wasanii kushindwa kuhimili kulipa ada ya Sh. 500,000(laki tano) Bi. Fissoo
alisema kifungu cha 8 cha sheria hiyo kinampa Waziri mwenye dhamana
husika kutoa msamaha wa malipo kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa
kiasi cha fedha hizo.
“Ada
wanayolipa wasanii ya Sh.500, 000 (laki tano) ipo toka siku za nyuma
ambapo Sheria namba 4 ya Filamu na Michezo ya kuigiza inampa mamlaka
Waziri husika kutoa msamaha kwa msanii mchanga atakayeshindwa kulipa ada
hiyo”.alifafanua.
Alisema kwamba msamaha wa ada ya sh. 500,000 utatatolewa
pale tu msanii atakapotoa taarifa kwa Waziri husika na mara baada ya
kujiridhisha ndipo msamaha utatolewa na kutangazwa kwenye gazeti la
Serikali.
Amewashauri
wasanii wa Filamu kuwa Wazalendo kwa kutengeneza filamu zenye maadili
ya Mtanzania na si kutengeneza Filamu zenye maudhui ya kimagharibi.



Mwandishi wetu
NYOTA
imeanza kung’ara kwa mbunifu wa mavazi anayekuja juu jwa kasi nchini,
Doreen Estazia na lebo yake ya Estado Bird baada ya kupata kualikwa
kuhudhuria mkutano wa kujadili masuala ya Uchumi duniani (World Economic
Forum) utakaonza kesho mjini Devos –Klosters, Uswisi.
Estazia
ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliibuka na mavazi yaliyojulikana kwa
jina la What’s Your Freedom (WYF?) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya
Uhuru wa Tanzania alisema kuwa amealikiwa kama mjasiliamali katika
masuala ya ubunifu wa mavazi na atakuwa chini ya Global Shapers.
Alisema
kuwa hii ni faraja kubwa kwake kwani kipaji chake ndicho kimempa
nafasi hiyo na kuwa mbunifu wa kwanza nchini tokea taifa hili lizaliwe
kushiriki katika mkutano huo mkubwa.
Alifafanua
kuwa setka ya ubunifu wa mavazi inanulikana kimataifa kwani mbali ya
kupromoti nchi nje ya mipaka na hasa masuala ya vivutio vya utalii kwa
upande wa mavazi.
“Nashukuru
kupata nafasi hii na nitaiwakilisha vyema Tanzania, hii ni fursa pekee
ya kujitangaza kimataifa na hasa ukizingatia kuwa nimeanza kujihusisha
na masuala ya ubunifu mwaka mmoja uliopita,” alisema Estazia kabla ya
kuondoka juzi usiku.
Alisema
kuwa ameanza kupata mwanga wa mafanikio na lengo lake kubwa ni kufikia
hatua ya juu kabisa katika masuala ya ubunifu wa mavazi na wala si
viginevyo.
“Sina
malengo ya kuishia hapa hapa katika fani hii, nataka dunia inifahamu
kupitia ubunifu wa mavazi, mkutano wa Uswis ni moja ya njia ya kufikia
lengo kwani unawajumuisha pia wakuu wan chi mbali mbali duniani,”
alisema.

Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge
wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha
mchango wao kwa timu hiyo.
Benchi
la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu
ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga
kutoa kwa timu.
Mechi
hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni.
Twiga
Stars na Namibia zitapambana Jumapili (Januari 29 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania
tiketi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC)
zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.





No comments:
Post a Comment