Na Gladness Mushi -Arusha
MFUKO wa hifadhi ya jamii( NSSF)mkoani Arusha umefanikiwa kukusanya
shilingi bilioni 16.745 kwa kipindi cha Jully hadi desemba 2011 ambapo
fedha hizo ni sawa na asilimia 92 ya lengo walilokusudia
Hayo yalisemwa na meneja kiongozi wa mfuko huo mkoani hapa Bw Jackton
Ochieng' alipokuwa akiongea na gazeti hili kuhusiana na hali ya mfuko
huo .ilivyo kwa sasa.
Aidha alisema kuwa mfuko huo umeweza kuandikisha wanachama 3582
ambapo ni sawa na asilimia 49.8 ambapo hilo ndilo lengo hailsi
Vile vile aliongeza kuwa kwa kipindi hicho pia wameweza kuandikisha
waajiri 72 ambapo ni sawa na asilimia 79 ya lengo
Hata hivyo bw Ochieng' alieleza kuwa mfuko huo umeweza kulipa mafao
kwa wanachama wake 2416 ambapo kifedha wamelipwa shilingi bilioni
4033.65.
Alieleza changamoto zinazoukabili mfuko huo kuwa ni pamoja na watu
kutojua dhana ya elimu ya mfuko wa jamii na hivyo kuwafanya kuwa waoga
kujiunga na mfuko huo ambapo alisema kuwa hadi sasa wamejitahidi kutoa
elimu hiyo kwa waajiri 53 .
Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wafanyakazi
kurubuniwa na waajiri hali ambayo inaleta matatizo katika mfuko huo.
Aliwataka wanachama na wasio wanachama kutokubali kurubuniwa na
waajiri kwa kuwa ni haki ya mfuko kuhudumia wanachama wake kuanzia
sasa na hata uzeeni
No comments:
Post a Comment