

NA :Ramadhani Juma, Afisa habari wilaya ya Sumbawanga
VIKUNDI vya wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vimeanza kufaidika na miradi ya
kilimo kupitia Mashamba Darasa inayodaiwa kuwaongezea mbinu za kisasa
za kilimo bora hali inayotarajiwa kuwaongezea mavuno na kipato ikiwa ni
juhudi za kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini.
Baadhi
ya wanachama wa kikundi cha CHEMKA kilichopo katika kijiji cha Kaoze
kilichopo bonde la ziwa Rukwa walisema wamenufaika sana na elimu ya
mradi wa shamba darasa uliotekelezwa katika kijiji hicho na kwamba wamekuwa wakipoteza mazao mengi kwa kulima kilimo cha kiasili.
Walisema
kuwa, kwa kipindi kirefu wamekuwa wakivuna magunia matatu mpaka matano
kwa hekari moja walipokuwa wakilima kilimo cha asili lakini kwa kilimo
bora cha kisasa wanategemea kupata magunia 25 mpaka 30 kwa hekari moja
hivyo wanategemea kujiongezea kipato na kujikwamua katika umasikini.
Kwa mujibu wa
Afisa Kilimo wa wilaya hiyo Shaaban Bahari, Halmashauri hiyo ina jumla
ya mashamba Darasa 151 katika vijiji mbalimbali wilayani humo na
kwamba hali hiyo inatarajiwa kuwafaidisha wakulima.
“Tunategemea
miradu hii itawasaidia wakulima wetu kujiongezea mbinu mbalimbali za
kilimo cha kisasa ikiwemo matumizi ya mbolea, kupanda kwa kuzingatia
nafasi, pamoja na kutumia mbegu bora” alisema Juma.
Miradi
hiyo ya mashamba darasa inatekelezwa na wilaya hiyo katika vijiji na
Kata mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi wakulima wilayani humo,
ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea pamoja na mbinu nyingine za kilimo
cha kisasa.


No comments:
Post a Comment