NA GLADNESS MUSHI- ARUSHA
Kikundi
cha akinamama wapatao 50 kinaojishughulisha na biashara ya kuchoma
mahindi katika jiji la Arusha kinatarajia kuongeza kipato kupitia
biashara hiyo baada ya wanachama wake kupatiwa majiko yaliyosanifiwa kwa
tenknolojia ya kisasa.
Upatikanaji
wa majiko hayo yaliyotengenezwa kwa teknolojia ya aina yake unaelezwa
kuiongezea dhamani biashara hiyo ya uchomaji mahindi ambayo akinamama
wengi na vijana wamekuwa wakiifanya.
Kwa
msaada mkubwa wa mtandao wa vijana nchini,kikundi kinachofahamika kama
Wamama Wachoma Mahindi Arusha kimeweza kufadhiliwa na kupata majiko sita
yenye dhamani ya shilingi milioni mbili ambapo mwenyekiti wa kikundi
hicho Bi Sophia Juma anasema yatasaidia kuongeza ufanisi katika biashara
hiyo.
Mwenyekiti
wa mtandao wa vijana nchini YDN,Bw.Elipokea Urio amesema upatikanaji wa
majiko hayo ni sehemu ya mikopo midogomidogo ambayo imekuwa ikitolewa
na halmashauri ya jiji la Arusha katika kuinua vipato cha vya
wafanyabiashara wadogo na wakati.
Naye
Fundi aliyesanifu majiko hayo Bw.John Werema amesema kitaalamu aina
hiyo ya majiko ni rafiki wa mazingira kutokana na muundo wake
Biashara
ya uchomaji wa mahindi licha ya kutengeneza ajira kwa baadhi ya
kinamama na vijana imekuwa ikielezwa kuchangia uchafuzi wa mazingira
katika baadhi ya maeneo nchini lakini sasa aina hii ya majiko inaelezwa kuwa tiba sahihi katika kukabiliana na hali hiyo.
No comments:
Post a Comment