Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Siha,Bw.Rashid
Kitambulo akizungumza na kuishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo, mwisho kushoto ni Mwalimu mkuu wa sekondari ya Oshara
Elieta Kaaya akifatiwa na wawakilishi wa Airtel Pascal Bikomagu na
Jane matinde (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa sekondari Wilaya ya
Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika
shule ya sekondari Oshara jana.
Airtel yatoa msaada wa vitabu shule 4 za secondari wilaya ya SIHA - Kilimanjaro
Chini ya mpango wake wa Airtel Shule Yetu kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari
zilizoko wilaya ya Siha ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo.
Hafla hiyo fupi imefanyika katika shule ya sekondari Oshara ambapo
shule zilizonufaika na msaada huo ni za sekondari ya
Oshara,Kilingi,Magadini na Namwai zote za wilayani humo ambapo
wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa msaada huo na Mkurugenzi wa
Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Siha bw, Rashid Kitambulo ambaye
alikabidhiwa vitabu hivyo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya airtel bi,
Jane Matinde. kila shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya
shilling milio moja.
Akiongea katika hafla ya makabithiano iliyofanyika katika shule ya
sekondari Oshara Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde
alisema" Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia
wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa
sehemu ya maendeleo ya shule hizi 4 za sekondari wilayani Siha na
kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa
nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hizi”
“Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika
kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu
ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho” Aliongeza
Matinde.
Mgeni rasmi katika halfa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Siha bwana Kitambulio Rashidi alisema tunayo fuhara kuona Airtel
inajitoa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati
mikakati ya elimu halmashauri yetu iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba
kila nyumba moja ya mkazi wa siha anatoka graduate na ili kufikia
malengo yake kuna mahitaji ya vitabu vya kufindishia, tunashukuru sana
Airtel kwa kutusaidia katika kutimiza malengo tuliojiwekea
Bw Rashidi pia alichukua fulsa hiyou kuwaasa wanafunzi kuvitumia
vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi na kufikia
lengo halmshauri hiyo iliyojiwekea
Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa sekondari wilaya ya Siha Mussa
Shaabani Ally wameishukuru Airtel kwa kuwawezesha vitendea kazi na
kuongeza kuwa wilaya hiyo mpya bado inakabiliwa na changamoto nyingi
katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika
mambo mengine.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali
kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa
msaada wa kutoa computer 4 kwa shule ya sekondari mlangarini iliyoko
wilaya ya Arumeru mkoani na pia kuchangia katika sekta ya afya ambapo
Airtel iligawa baskeli kumi kwa vituo vya afya wilayani misungwi
Mkoani Mwanza. Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na
kuchangia katika huduma kwa jamii.
No comments:
Post a Comment