

Na Mwandishi Wetu
MALKIA wa muziki wa Injili nchini,
Rose Muhando, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha
la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Alex Msama, ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama
Promotions ya Dar es Salaam, Muhando amethibitisha kushiriki tamasha
hilo.
"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu
ndipo Rose Muhando atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya
Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe," alisema
Msama.
Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo
saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu,
Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando
pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya
Krismasi) na Jipange Sawa Sawa.
Msama alisema pia Muhando ataimba
pamoja na Anastazia Mukabwa wa Kenya aliyeshirikiana naye katika albamu
ya Vua Kiatu, na baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi
mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.
"Mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo
na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Muhando
atakuwepo na Mukabwa atakuja na kundi la waimbaji wake," alisema Msama.
Albamu ya Vua Kiatu inabeba nyimbo
nane ambazo ni Vua Kiatu uliobeba jina la albamu hiyo, Ee Mungu, Usiwe
Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme.
Mbali na Mukabwa, wengine
waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya
Pasaka ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho wa Dar es
Salaam, kundi la Glorious Celebration na Atosha Kissava kutoka Iringa.
Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo
baada ya kufanyika Dar es Salaam, pia litarindima kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu.
Tamasha la mwaka huu malengo yake
makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na
kuwasaidia mitaji wanawake wajane.
Kiingilio katika tamasha hilo
kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh.
5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia
litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika
ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.

The Girl Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”,
aimed at empowering Secondary school girls
Saturday 10th March 2012, As part of our Corporate Social
Responsibility initiative, Airtel Tanzania has today launch ”The Girl
Empowerment Program” under the theme ” Build Your Future”, aimed at
empowering Secondary school girls aged 14 to 18 years, in achieving
their future career goals and build self confidence amongst young
women.
The Girl Empowerment Program is key to Airtel as it goes hand in hand
with Airtel’s mission of educating the girl child and creating brand
loyalty. Apart from the fact that they need clear rules, consistent
consequences for breaking rules and encouragement to do their best,
young girls need opportunities outside of school curriculum to learn
and develop new skills and interests with other youth and adults.
Speaking during the launch held at Canossa Girls Secondary School in
Tegeta, Dar es Salam Airtel customer Care Director Adrianna Lyamba
said ”Today we kick start the program this quarter with “Canossa
Girls Secondary School in Tegeta, The Girl Empowerment Program will be
an ongoing program which will be done quarterly to Girls Secondary
Schools around Tanzania and in this program we will be covering
different topics relating to career management, building self
confidence and making the right decisions in life.
We will be
requesting our own employees to volunteer to speak in schools and
share their career experiences and skills with the students. This will
enable the students understand what it takes to build a career and
select the right career path in life”.
“There is the say that saying, when you educate a women you have
educated the whole community, we therefore believe the knowledge
acquired will be a great significance to girl’s destiny and for the
upcoming generation. She added
We are highly committed towards supporting Tanzanian community, apart
from Girl empowerment program we have been supporting education sector
through Shule yetu program were we provide books to Secondary schools
in the country, our aim is to improve education level through
availability books to secondary schools students. Since we started our
books support programme, approximately seven years ago, we have
reached more than 800 secondary schools that are spread across the
country”

Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Azam lililochezwa Machi 10
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 72,731,000.
Jumla
ya watazamaji 19,339 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa
kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya
rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh.
15,000.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 11,303,932.20 kila timu ilipata
sh. 14,726,592.20, uwanja sh. 4,908,864.07.
Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,963,545.63, TFF
sh. 4,908,864.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,454,432.03, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 490,886.41 na
asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 4,908,864.07.
Gharama
za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000,
nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. waamuzi wa akiba sh.
30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, tiketi sh.
3,540,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000,
usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing
Construction) sh. 2,000,000.
Gharama
nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu
ilipata tena sh. 1,353,730 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 1,160,340.
Saturday, March 10, 2012

Mwanzo ulikuwa ni
mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo
yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna
Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo
ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima
aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo
ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae
naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na
vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.
Hali ilikuwa kama hivi angalia matukioo ya picha hizi.

(PICHA KWA HISANI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO)
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezitaka kampuni na taasisi zinazohusika na kutoa huduma muhimu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Julius Kambarage Nyerere ziharakishe kufanya hivyo ili ujenzi wake ukamilike mapema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Machi 10, 2012)
mara bada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo hicho na kukagua ujenzi
wake katika mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.
Kampuni
zinazotakiwa kufanya hivyo ni TANESCO kwa ajili ya umeme wa jengo hilo,
Kampuni ya Simu (TTCL) kwa ajili ya mkonga wa mawasiliano na Idara ya
Kodi ya Mapato (TRA).
Waziri Mkuu amesema ujenzi
wa kituo hicho cha mikutano ni ishara ya urafiki wa muda mrefu
ulikuwepo baina ya Tanzania na China na kwamba kukamilika kwake
kutaboresha mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Mapema,
akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo ambalo litagharimu yen milioni
183.5 sawa na dola za Marekani milioni 30, Balozi wa China nchini
Tanzania, Bw. Lv Youqing alisema ujenzi wa jengo hilo ulianza mara baada
ya sherehe za uzinduzi Januari 15, 2010.
Awali,
ujenzi wa jengo hilo ulitarajiwa kukamilika Aprili, 2012 lakini
kutokana na uchelewashaji wa miundombinu hiyo muhimu hivi sasa
linatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu.
Litakapokamilika
jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 1,000; litakuwa
na kumbi ndogo ndogo nne zenye uwezo wa watu zaidi ya 20, ukumbi wa
chakula wa watu zaidi ya 700 na ofisi za watumishi wa ukumbi huo.
Vilevile, kutakuwa na ukumbi mmoja ambao unaweza kugawanywa
(partitioned) na kutengeneza ofisi za muda kwa watu wanaoendesha mkutano
mkubwa katika ukumbi huo.
Naye
Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho, Bw. Huang Meiluan alisema
ujenzi wa ghorofa ya chini umekamilika kwa asilimia 40 kwa sababu bado
wanasubiri huduma muhimu zikamilike ili waanze kuweka sakafu.
“Tunasubiri kuunganishwa na mkonga wa mawasiliano wa Taifa, bado
hatujaweka njia kuu za umeme za kuingia katika jengo... kasi ya ujenzi
imeathirika kutokana na kutokamilika kwa huduma hizi muhimu,” alisema.
Alisema
ujenzi wa ghorofa ya kwanza na ya pili umekamilika kwa asilimia 90 na
imebakia kazi ya kumalizia kuweka nakshi za ndani tu (interior
decoration). “Kwa nje, kazi ya ujenzi imekamilika na tumeanza kuweka
nakshi, kazi hii imekamilika kwa asilimia 75,” alisema.
Alisema
wanakabiliwa na changamoto ya wizi wa vifaa vya ujenzi unaofanywa na
vibaka kila mara na kwamba inawapa mtihani kwani itawalazimu kuagiza
upya vifaa hivyo kutoka China. Aliomba polisi wawasaidie kuimarisha
ulinzi katika eneo la ujenzi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe
alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imeanza kushughulikia
upatikanaji wa kifaa muhimu cha umeme ambacho kilishindwa kupatikana
hapa nchini.
Alisema
vyuma vilivyotumika katika hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho ni
tani nyingi, na kwamba yanahitajika malori ya kuvisomba na kibali kutoka
TRA ili yaweze kupelekwa katika eneo jingine kwa kuhifadhiwa.
Alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba wizara yake inafuatilia suala hilo
pia.
Kuhusu
uwekwaji wa nyaya za mkonga wa mawasiliano ambao unapaswa kufanya na
TTCL, waziri Membe aliomba apewe wiki moja zaidi kwani amekuwa
akisumbuana nao kwa zaidi ya mwezi mmoja bila mafanikio yoyote. Suala la
ulinzi pia alisema ameshaanza kulishughulikia.



Hafla hiyo inafanyika katika ofisi za Multichoice zilizopo Saint Peter Oysterbay jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi
Diana Kimaro wa Chuo Kikuu cha Nilai Malasia akisomea masuala ya
biashara ambaye yuko katika benki ya NMB kwa mazoezi akimpatia huduma
mmoja wa wateja wa benki ya NMB aliyefika katika hafla hiyo, Benki ya
NMB pia imeshiriki katika hafla hiyo kwa ajili ya kuwaelezea wateja wao
huduma mbalimbali wanazozitoa.



Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara Jana (Machi 10 mwaka huu) amechangia sh. milioni moja kwenye uzinduzi wa
akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ambayo
inashiriki michuano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC).
Akizungumza
kwenye hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam, Dk. Mukangara alisema ni
jukumu la kila Mtanzania kuichangia Twiga badala ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuachiwa pekee mzigo huo wa kuendesha
timu hiyo.
Wachangiaji
wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba 13389 ambapo
kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala (transaction) mmoja
ni sh. 500,000. Kwa Waziri Dk. Mukangara kuchangia sh. milioni moja
alifanya mihamala miwili.
Naye
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema Twiga Stars
kwa sasa haina mdhamini na Shirikisho limekuwa likibeba mzigo wa
kuhakikisha inashiriki katika mechi za kirafiki na mashindano mbalimbali
kwa vile imekuwa ikifanya vizuri.
Twiga
Stars inayofundishwa na kocha Charles Boniface Mkwasa iko kwenye
raundi ya pili ya mashindano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis Ababa.

Mkurugenzi
Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania
Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya
Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara
inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC)
kupitia Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm). (Pichana
Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Shirika hilo linafadhili ujenzi wa
barabara kuu za lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224
kwa miradi ya Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa
mujibu wa Bwana Mchomvu miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote
kuzingatiwa itakuwa imekamilika ifikapo mwezi June 2013 na barabara
zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi wa nane 2013.
Kwa upande wa Ruvuma shirika hilo
linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea kuelekea Wilaya ya
Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika mwakani.
Hata hivo Mkurugenzi huyo
aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa
kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa
vifaa vya ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa
vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na
wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa jitihada zao
za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi
karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi
muhimu kwa wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku
hususani kuwaunganisha na kituo cha afya cha Laela.

No comments:
Post a Comment