Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akipokea ufunguo wa moja
ya gari kutoka kwa mwakilishi wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga
(kushoto) ikiwa ni ishara ya kukabidhi msaada wa gari 4 na pikipiki 20 vyenye
thamani ya Tsh. Milioni 261 leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi akiwasha moja ya kati ya magari
manne aliyoyapokea kutoka kwa mwakilishi
wa shirika la GLRA la Ujerumani nchini Burchard Rwamtoga leo jijini Dar es
salaam.
Mwakilishi
wa shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) akimkabidhi Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) ufunguo wa moja kati ya
pikipiki 20 zilizotolewa na shirika la hilo leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akimkabidhi Mratibu wa
huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Kigoma Dkt. Deus Leonard (kushoto) moja
kati ya magari manne yaliyokabidhiwa kwa
Serikali kutoka kwa shirika la GLRA la
Ujerumani nchini leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na Mratibu
wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa Ilala baada ya mkabidhi moja kati ya
magari manne yaliyokabidhiwa kwa
Serikali kutoka kwa shirika la GLRA la
Ujerumani nchini leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).
No comments:
Post a Comment