TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 25, 2014

Pinda ataka urais

  • Atumia mgongo wa Ikulu na viongozi wa dini
  • Ataja watano watakaopenya Kamati Kuu, NEC
Pinda ataka urais 
WAKATI makada watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitumikia adhabu ya mwaka mmoja kwa kosa la kuanza kampeni za urais wa 2015 kabla ya muda, Waziri Mkuu Mizengo Pinda naye anadaiwa kutangaza kusudio la kuwania urais,
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Pinda alitangaza nia yake katika kikao cha wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka mikoa sita ya kanda ya Ziwa, alichokiitisha juzi jioni Ikulu ndogo jijini Mwanza.
Katika kile kinachoonekana kama amepangwa rasmi kimkakati, Pinda aliwaeleza wajumbe hao kwamba hakuwa na nia ya kugombea lakini ameshawishiwa na baadhi ya maaskofu, masheikh, mkewe pia na anaungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete.
“Waziri Mkuu alituita juzi sisi wajumbe wote wa mkutano mkuu Taifa kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa. Tuliitikia wito tukakutana naye hapo Ikulu ndogo ya hapa Mwanza.
“Hakukomea hapo, bali alituambia kuna majina ya watu watano bora akiwemo yeye, Edward Lowassa, kijana, mwanamke na Mzanzibari kuwa ndiyo watakayopitishwa na Kamati Kuu kwenda NEC,” kilieleza chanzo chetu.
Ingawa Pinda hakupatikana kwa simu kuzungumzia madai hayo, ila mtoa taarifa hizo ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho, alisema kuwa kada huyo wa CCM alijivunia utumishi wake wa muda mrefu Ikulu tangu mwaka 1974.
Kwamba, alisema kuwa hatakuwa rais wa kutumia fedha chafu kuhonga wajumbe kama wanavyofanya baadhi ya wanasiasa wengine, bali atatumia fedha za marafiki zake kuwasaidia wale wote watakaomuunga mkono.
Inaelezwa kuwa kila mjumbe alipewa posho ya sh. 50,000 kwa ajili ya nauli, chakula na malazi kwa siku moja, kiwango ambacho hata hivyo kimelalamikiwa na wajumbe wakidai ni kidogo.
“Hadi makatibu wa CCM wilaya za mkoa wa Mwanza wamepewa maelekezo na kigogo mmoja wa mkoa ili wamuunge mkono Pinda katika safari yake ya kuutaka urais,” alisema na kuongeza;
Pinda amelazimika kukutana na wajumbe hao ili kujenga ushawishi kwao, kwa sababu anahofia nguvu kubwa ya kukubalika Lowassa ndani ya chama katika mbio hizo za urais 2015.
“Tulipomaliza kikao na Pinda pale Ikulu na kutoka nje, wajumbe wengi walipuuza mpango wake huo wakidai hafai kuwa Rais. Walisema kwanza yeye mwenyewe hana nia ya kugombea ila ameshawishiwa tu.
“Pili, wajumbe walihoji Pinda ni mjumbe wa Kamati ya Maadili, NEC na Kamati Kuu ya chama, aliyeshiriki kuwafungia Lowassa, Stephen Wassira, January Makamba, Bernard Membe, Fredrick Sumaye na William Ngeleja kwa miezi 12 kutokana na kukiuka taratibu na kaunza kamapeni mapema, kwamba yeye itakuwaje,” kilisema chanzo hicho.
Pinda aliingia jijini Mwanza juzi na kwenda kumhani Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga aliyefiwa na mtoto wake, Vedastus Kitwanga na jana usiku aliongoza harambee ya Taasisi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Mwanza. CHANZO >>>>>>

No comments:

Post a Comment