Kaimu
Katibu Tawala wa wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akitoa ufafanuzi kwa wajumbe
wa maandalizi ya shughuli ya uzinduzi wa Programu ya uimarishaji wa mipaka ya
Kimataifa wa wilaya ya Ngara itakayozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete eneo la
Mugikomero mpakani mwa Tanzania na Burundi. Wanaoonekana nyuma ni raia wa Burundi
waishio mpakani.
Raia wa
Burundi wakiwa nyuma ya alama ya mpaka inayotenganisha
Tanzania na Burundi. Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi inaendelea na zoezi la kuhuisha mipaka hiyo ya kimataifa.
Moja ya Shamba
la ndizi lililopandwa katikati ya eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi
ambalo kwa sheria za kimataifa haliruhusiwi kufanyiwa shughuli yoyote.
Bw. Israel
Paul akipaka rangi moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi eneo
la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa
mipaka ya kimataifa.
Viongozi wa wilaya ya Halimashauri ya
Wilaya ya Ngara wakikagua moja ya eneo la mpaka wa Kabanga unaotenganisha
Tanzania na Burundi ambapo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania atampokea Rais wa Burundi
Pierre Nkurunziza.
Moja ya alama ya mpaka unaotenganisha Tanzania na Burundi ikiwa imekamilika katika eneo
la Mugikomero, wilayani Ngara kufuatia Programu inayoendelea ya uhuishaji wa
mipaka ya kimataifa.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO
26/8/2014. Ngara, Kagera.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa kwa lengo
la kuhuisha alama zilizopo na kuweka mpya katika maeneo ya mipaka ya Tanzania ambayo awali yalikuwa
yametengwa na mito na baadaye mito hiyo kukauka .
Programu hiyo
inayofanywa na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itazinduliwa
rasmi Agosti 28, katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero
wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare kwa upande wa Burundi.
Aidha, itahusisha ujenzi na uwekaji wa vigingi
vya mipaka, Marais wa nchi za Burundi na Tanzania kutembelea baadhi ya maeneo
yenye alama za mipaka na kisha kuzungumza na wananchi waishio mpakani.
Katika tukio hilo Rais
Jakaya Kikwete anatarajia kumpokea mwenzake wa Burundi, Rais Pierre Nkurunziza
atakayewasili nchini Tanzania kushuhudia zoezi hilo akitokea nchini Burundi kupitia
mpaka wa Kabanga ulioko wilayani Ngara.
Kaimu Katibu Tawala wa
wilaya ya Ngara Bw. Hussein Seif akizungumzia maandalizi ya shughuli hiyo amesema
kuwa wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa programu hiyo inatekelezwa kwa
ufanisi katika maeneo yote ya wilaya ya Ngara yanayopakana na nchi ya Burundi.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi wa Topographia na Giodosia wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt. James Mtamakaya akizungumzia zoezi hilo amesema kuwa tayari maeneo
mbalimbali ya mipaka ya Tanzania yameshapitiwa na zoezi hilo likiwemo eneo la
mpaka kati ya Tanzania na Uganda.
Ameyataja
maeneo
mengine kuwa ni eneo la Tanzania na Rwanda ambalo bado linatenganishwa
na mto Kagera, eneo la mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji, Tanzania na
Kenya pamoja na
zoezi la uimarishaji wa mpaka kati ya Burundi na Tanzania ambalo
linaendelea
kufanyika.
No comments:
Post a Comment