Kaimu
mwenyekiti wa Uukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda akizungumza
na wanandishi wa habari leo Agosti 27, 2014 juu ya mwenendo wa bunge la
katiba.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Wakati
mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu
sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo, nao
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) wazidi kumtupia lawama zote za
kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mheshimiwa Samweli Sitta
na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge
hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza
na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa Jukwaa
la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda amesema kuwa JUKATA wamekuwa
wakifuatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na
kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha
wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia
taifa katiba mpya ya watanzania.
Wanahabari
mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano Bw
Mwakadenga amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki
katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya
kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika
kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema
kuwa ni wizi mpya kwa
watanzania,
“Kwanza
bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini
uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika
na kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100
tuligundua kuwa hawapo bungeni wakiwemo mawaziri wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya
viongozi wa kamati”amesema Mwakagenda.
Ameongeza
kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya bunge hilo kuvurugika ni pamoja
na kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa, matumizi mabaya
fedha ikiwa ni pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni,
kukosekana kwa theluthi mbili toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja
na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye rasimu mambo ambayo amesema kuwa
mwenyekiti Samweli Sitta ameyafumbia macho na kijifanya kama hayaoni
huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.
“Huyu
mzee hatujamwelewa kabisa, sisi tumekaa tumezungumza naye tukamuuliza
atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe watapatikana wapi hajatupa
jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambayeameshachanganyikiwa,
anapambana na kila anayekuja mbele yake, iwe mwandishi, mwanaharakati,
mbunge, yeye amekaa kujihami tu, sasa hali hii sio nzuri kwa mchakato
muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika
hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi Kikwete kiusimamisha mchakato
huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na kuonekana wazi kuwa
hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi ambayo sisi
kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba bora,
“Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
“Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.
Mchakato
wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma bila ya mariano na wajumbe
waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais amekubali kukutana
nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato huu.
No comments:
Post a Comment