Mkuu wa matawi (Cluster Head) wa Benki ya Exim Tanzania, Bi
Agnes Kaganda (wapili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw.
Abdul Kuratasa kwapamoja wakifungua jiwe la msingi kuonyesha makabidhiano rasmi
ya maliwato iliyojengwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Kaka Mkuu wa Shule Seif
Ahmed (wa kwanza kushoto), Dada Mkuu wa shule Naomi Shakila (wa kwanza kulia)
na mlezi wa shule hiyo Dkt. Ellen Otaru (wa pili kulia). Na mpiga piga wetu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw. Abdul Kuratasa
akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maliwato iliyokabidhiwa na Benki ya Exim
Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es
Salaam.
======== ======= ======
BENKI
ya Exim Tanzania imekabidhi vyoo vya kisasa kwa Shule ya Msingi Kilakala
iliyopo katika wilaya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za
benki hiyo kuboresha hali ya usafi na mazingira ya kujifunzia shuleni
hapo.
Ujenzi
huo wa matundu kumi ya vyoo na mfumo safi wa maji ni moja kati ya
miradi ya kimaendeleo iliyotekelezwa na kugharamiwa na Benki ya Exim
Tanzania katika shule hiyo ya Kilakala iliyo chini ya benki tangu mwaka
2012 ikiwa kama benki mlezi.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano shuleni hapo jana Mkuu wa
Matawi/Cluster Head wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda, alisema benki yake
imeamua kupiga jeki mradi huo ikitambua umuhimu wa usafi kwa afya ya
wanafunzi na walimu na mchango wake katika maendeleo kitaaluma kwa shule
hiyo.
“Shule
ilikuwa na maliwato yenye matundu nane tu ikiwa na wanafunzi 2739.
Kutokana na Benki ya Exim kuongeza matundu mengine kumi, tunaamini kuwa
hali hii sasa italeta ahueni kwa wote, walimu na wanafunzi hapa
shuleni,” alisema.
Alisema
kuwa mbali na matundu hayo kumi, wavulana nao wana sehemu maalum ya
maliwato ikiwa na maji yanayotembea ili kuiweka maliwato katika hali ya
usafi muda wote.
“Tunaamini
kuwa, kwa kuboresha hali ya usafi ya shule kutasaidia kuzuia wanafunzi
haswa wasichana kutoruka vipindi vya masomo ili kutafuta vyoo visafi au
wanafunzi kutoambukizwa magonjwa ya kuambukizwa. Hii itawasaidia wao
kuelekeza zaidi jitihada zao katika masomo, na hivyo kuweza kufanya
vizuri zaidi darasani,” alisema Kaganda.
Alibainisha
kuwa sasa ni juu ya uongozi wa shule na jamii inayoizunguka shule
kuhakikisha kuwa maliwato hiyo inatumika vizuri ili iweze kutumika na
wanafunzi wengine wanaoweza jiunga na shule hiyo siku za usoni.
“Ningependa
kuuasa uongozi wa shule na wanafunzi kuhakikisha kuwa maliwato hii
inatunzwa na inabaki kuwa safi. Lengo hili litatimia tu endapo tutaweza
kuiweka maliwato yetu katika hali ya usafi,” aliongeza.
Alibainisha
kuwa Benki ya Exim imekuwa ikiibadilisha shule taratibu tangu ilipokuwa
benki mlezi, ambapo sasa shule hiyo inajivunia kuwa na maktaba ya
kipekee, wanafunzi wakisoma wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na
benki, na sasa shule ina mfumo nzuri wa maji safi, vikitajwa kwa
uchache. Miradi yote ikifadhiliwa na benki kama sehemu yashughuli mbali
mbali za kijamii.
Naye,
mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw. Abdul Kuratasa alipongeza jitihada za
benki katika kufuatilia maendeleo ya shule tangu ilipoichukua kama benki
mlezi na kusema kuwa sasa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kilakala
wanafurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama shule nyingine za
binafsi.
Alisema
kuwa mchango huo wa maliwato ni moja kati ya hatua ambazo zinapaswa
kuigwa na makampuni mengine ili kuboresha sekta ya elimu nchini.
“Naipongeza
benki kwa jitihada zake kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya
kujisomea ya shuleni hapa. Dhamira ya benki katika kusimamia maendeleo
ya shule imekuwa thabiti tangu ilipoichukua shule yetu kuwa benki mlezi
mnamo Agosti mwaka 2012.
“Tungependa
kuishukuru Benki kwa kutujengea maliwato na tunahaidi kuwa tutaitunza
vyema kwa ajili ya wanafunzi wengine katika siku za usoni,” alisema Bw.
Kuratasa.
No comments:
Post a Comment