Tanzania kama inavyofahamika kwa Wakati huu, ipo katika Harakati mbaya sana za kuhakikisha inapigania Vitu Viliwi vikuu, moja ikiwa kupata Katiba Mpya itakayoendana na Matakwa ya Watanzania, na pili kuhakikisha inapata Rais Mpya wa AWAMU YA TANO, ambaye watanzania wanadhani ndiye mkombozi haswa wa Taifa hili Tokea Kipindi cha Mwalimu.
Katika Kuhakikisha kwamba Tanzania inapata mambo hayo yote hivi sasa kumekuwa na harakati mbalimbali kutoka kwa watanzania wenyewe ikiwa ni pamoja na hawa ambao kwa sasa wapo kwenye mchakato mzima wa kuwania nafasi hizi za nyazifa wanazotaka wao.
lakini wakati wakifanya hivyo pia jamii yote kwa sasa imekuwa ikitoa misukumo na michango yake kwao kuhusiana na utendaji wao wa kazi pindi wanapochaguliwa lakini pia kumekuwapo na msukumo mkubwa kwa jamii yenyewe, imeanza kujitambua na kuanza kutaka haki za msingi ikiwa ni pamoja na kutaka katiba iwe ya wazi kwa ajili ya manufaa ya jamii na si manufaa ya Viongozi.
jambo hili ni gumzo sana kwa Mataifa mengi, pamoja nakwamba hadi sasa hakuna Nchi ambayo inaweza kusema kile kinachoweza kutokea kwa Tanzania kutokana na harakati hizi maana Watanzania wengi wanaoishi katika ardhi ya Tanzania na wale wanaoishi katika Mataifa mengine, wamepevuka zaidi kutokana na Dunia yenyewe, hivyo wakati mwingi wamekuwa wafuatiliaji wa masuala ya Kitaifa na kimataifa ususani katika suala zima la harakati hizi za mwanya huu wa kuwania hizo nyazifa.
baadhi ya Wachoraji pia wapo mstari wa mbele kuhakikisha kwamba wanafikisha ujumbe wao kwa Taifa, lakini pia kuna idadi kubwa ya Wandishi ambao pia wanafikisha Taarifa zao kwa Karamu zao kuelezea hisia zao na mstakabali unaoweza kuitokea Tanzania endapo watashindwa kufia makubaliano ya Mambpo yaliyopo mbele yake.
Kuna Mengi yamesemwa sana na Pia Matukio mengi yamejitokeza katika kipindi hiki cha Awamu ya Nne ikiwa ni vuguvugu la Kisiasa na kiuchumi, Watanzania wengi kwa sasa wanasubiri kusikia vyama vikijitokeza kuweka wazi wagombea wao, ambao bila sha huu utakuwa ni uchaguzi wa kwanza kuwa mgumu kwa Tanzania, kwa kuwa hivi sasa watanzania wamechoka na ule ulaghai waliokuwa wakiewa wakati huo na Viongozi.
ni uchaguzi Mgumu kwani pia idadi ya Mambo yaliyobadilika kidunia ni mengi na ambayo wameyashuhudia kutoka nchi za jirani, na pia nchi zingine za mbali, lakini kubwa itakuwa ni nani hanastaili kuwa kiongozi Bora( RAIS WA TANZANIA) nafasi hiyo kwa Aawamu hii ya tano ni kitendawili kwa Watanzania wote, kutokana na vyama vya Siasa kuinuka na kuwa na changamoto za maendeleo kwa chama Tawala.
Chama Tawala kina wakati mgumu ukilinganisha na kipindi cha miaka ya nyumba ambapo watanzania wengi walikuwa bado hawajatambua nini Umuhimu wa Uchaguzi, lakini kutokana na maisha kubadilika wameweza kubadilika pia na kutambua thamani ya nchi.
Kwani miaka ya nyumba watanzania wengi hawakufahamu maana na thamani ya Tanzania katika uchumi wao na uchumi wa Taifa, Miongo minne iliyopita Watanzania walikuwa wameendelea kuongozwa kwa kufuata katiba iliyokuwa imefichwa kwa Watanzania Wenyewe, hivyo baada ya kuwapo na kuibuka kwa hivi vyama vya Upinzani, hata Serikali iliyopo Madarakani pia kupitia Viongozi waliopo, wameweza kupata misukosuiko ya hapa na pale, ikiwa ni pamoja na kuwajibishwa kwa utendaji wake mbovu kutoka vyama pinzani.
Vyama vya Upinzani mpaka sasa vipo katika jitiada za kutaka kuiondoa Serikali iliyopo Madarakani inayotokana na Chama Tawala cha CCM, lakini maswali mengi kwa Watanzania ni kwa jinsi gani Wanaweza kuitoa madarakani hiyo Serikali kwani Watanzania wenyewe kwa wenyewe wanafahamiana, Tangu Enzi hizo, na ndiyo maana utasikia hii leo Kiongozi huyu kaondoka CCM kakimbia chama Pinzani ama kaondoka Chama Pinzani kakimbilia chama Tawala.
Hali hiyo inaonyesha ni kwa namna gani Watanzania wenyewe wanajitambua kwa Nafasi zao, inawezekana chama Tawka kikawa bado ni bora isipokuwa ndani ya chama hicho kuna watu ambao siyo Viongozi Bora, na watanzania wanatambua hilo hivyo inawezekana pia Chama Tawala kuteua Mgombea ambaye anakubaliwa na Watanzania wenyewe na Kikazidi kutawala maana Uchaguzi wa Watanzania wakati wote wanataka Kiongozi Bora.
lakini pia inawezekana ndani ya chama Tawala watanzania wakashindwa kupata Mtu ambaye anaweza kuwa kiongozi Bora , hivyo maamuzi yakafanyika ndani ya Vyama vya Upinzani na kupata kiongozi ambaye ni Sahihi na Chaguo la Watanzania.
Kwa habari zaidi kuhusu Uchaguzi wa Viongozi katika Tanzania katika kipindi cha mwaka 2015 ni Matukio na habari ambazo zinapatikana katika Mitandao ya:-
www.baloziwademokrasiatanzania.blogspot.com
www.missdemokrasia.blogspot.com
No comments:
Post a Comment