Na: Violeth John (DACICO TANZANIA).
Bendi ya muziki wa Mwambao (Taarabu) Mashauzi classic, siku ya jumamosi ya tarehe 30/8/2014 wiki hii,
itashuka kwenye Ukumbi wa Kisasa wa Nawina Resort Mbagala kuu ambako
wanatarajia kwa Mara ya kwanza kuwapa raha Mashabiki kwa kibao kipya cha
Asiyekujua Akuthamini.
Akizungumza mapema hii leo Meneja wa Mashauzi Classic Bw. Ismail
Rashid (Suma Ragar) amesemakuwa maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya
onyesho hilo siku ya jumamosi katika Ukumbi wa Nawina Resort uliopo mbagala
kuu.
“tunatazamia kuwapa raha Mashabiki wetu wa mbagala kuu,
kutokana na vibao vinavyozikoga nyoyo mashabiki wetu, katika Ukumbi wa Nawina
Resort kila tunapopeleka burudani mashabiki ujitokeza kwa wingi kiasi cha
kuleta msisimko wa hali ya juu, lakini hata hivyo awamu hii tumeamua kuwapa
kitu kipya kibao ambacho kinasema asiyekujua hakuthamini ulioimbwa na nyota
nguli wa Muziki wa Taarabu aisha Mashauzi” amesema Suma Ragar
Naye mkurugenzi wa
Nawina Resort, Mama Mary Komba, amesema
kuwa kwa Upande wa maandalizi kuhusiana na burudani hiyo, kila kitu
kimekamilika hivyo Wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake wajitokeze kwa ajili ya
kufika kupata burudani hiyo ambayo inapatikana kwa musimu kutokana na Aisha
kuwa na Ratiba ndefu ya burudani katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.
“kama unavyofahamu tena kwa sasa baada ya Mfalme wa Muziki wa
Taarabu, Mzee Yusuph Kuachana na aina ya huu muziki, kwa sasa hakuna shaka
kwamba Mashauzi ndiyo bendi pekee inayoendelea kutingisha katika Ulimwengu wa
Miziki ya Mwambao yaani Taarabu, kwa hiyo ninachukua fulsa hii kuwakaribisha
sana mashabiki wote wa Mashauzi Clasic siku ya jumamosi katika ukumbi wetu wa
Nawina Resort, ili wafike kusikia Vibao Vipya ukiwemo huu wa asiyekujua
hakuthamini, pamoja na nyimbo nyingine nyingi, lakini pia nichukue fulsa hii
kuwaeleza mashabikim kuwa, Usalama wa Magari pamoja na Vifaa vyao umeandaliwa
wa kutosha hivyo hakuna shaka kuhusiana na suala zima la ulinzi” amesema Mama
Mery Komba.
Vibao vingine vinavyotarajia kuitikisa mbagala Kuu siku hiyo
ni pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani,
Haya ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao
kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Kiingilio katika Onyesho hilo kimepangwa cha kuridhisha
kutokana na hali ya maisha ya wakazi wa eneo la Mbagala na Vitongoji vyake
ambapo kiingilio kimepangwa mlangoni shilingi 7000. Burudani hiyo inatarajia
kuanza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment