Moses Mashalla,
Mahakama
kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru
mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini
Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa
na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance
Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya
hoteli hiyo.Mbali
na agizo hilo mahakama hiyo pia imeagiza washtakiwa wanne kati ya
watano katika kesi hiyo walipe kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha
hizo tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi kingine cha asilimia 7
tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.
Hukumu
ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Robert
Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada ya kueleza kuridhika na
ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake
Melkizedek Lutema.
Katika
kesi hiyo iliyopewa usajili wa nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza
kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni sawa na sh,3 bilioni baada ya
kupatiwa hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja
kubainika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu.
Katika
hati ya madai mlalamikaji anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na
mkopo wenye riba wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo
hapa nchini na baada ya kugundulika hilo ilikwamisha biashara ya
mauziano ya hoteli hiyo.
Kwa
mujibu wa nakala ya hukumu iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa
watano katika kesi hiyo mshtakiwa wa kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick
Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa mshtakiwa wa kwanza Irene Tarimo
pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife Safaris Ltd wameamriwa
kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi cha riba hadi tarehe ya kukazia
hukumu.
Mbali
na agizo hilo washtakiwa wote katika kesi hiyo pia waliamriwa kulipa
gharama za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma huku
wakipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30 tangu hukumu hiyo
ilipotolewa.
Akihojiwa
jijini Arusha wakili wa upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao
wameridhika na hukumu hiyo na kwa sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama
za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma mnamo Januari 5
mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment