Mkuu
wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza na wanafunzi wa
Makete Girls Sekondari (hawapo Pichani) na pia kutoa maagizo kwa uongozi
wa shule.
Shule
ya sekondari ya wasichana (Makete Girl's) imetii agizo la mkuu wa
wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro la kutaka wanafunzi hao wapewe uji
mara baada ya vipindi viwili vya asubuhi badala ya saa nne agizo
alilolitoa Agosti 8 mwaka huu
Hali
kadhalika mkuu huyo aliagiza wapewe chakula cha mchana saa saba ili
kuweka uwiano mzuri wa muda wanaokula wanafunzi hao wawapo shuleni hapo
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa shule hiyo.
Mwandishi
wetu aliyefika shuleni hapo ijumaa ya Agosti 22, ameshuhudia maagizo
hayo yakitekelezwa jambo ambalo limepongezwa kwa kiasi kikubwa na
wanafunzi hao
"Ni
kweli tumeshuhudia ratiba ya chakula ikibadilika kama alivyoagiza mkuu
wa wilaya aliyokuja hapa shuleni, na kweli tunaona ni afadhali na
tutajisomea vizuri na limetekelezwa mara tu alivyoagiza hivyo naupongeza
uongozi wa shule kwa kutekeleza hilo" alisikika akisema mwanafunzi
mmoja
Katika
hatua nyingine shirika la sumasesu limetoa elimu ya ujinsia kwa
wanafunzi hao na kuwataka kujiepusha na vitendo vya ngono ilihali wao ni
wanafunzi ili waweze kufikia malengo yao
Rai
hiyo imetolewa na Bi Anifa Mwakitalima na kusema kuwa wao ni wanafunzi
wa kwanza katika shule hiyo na wanategemewa kufaulu na kuweka sifa nzuri
kwa wilaya, hivyo itakuwa nia aibu kubwa kwa mwanafunzi kuweka historia
ya kuwa mwanafunzi wa kwanza kusoma katika shule hiyo na pia akawa wa
kwanza kupata mimba na kufukuzwa shule
"Ninani
anayependa awe wa kwanza kupata mimba na kuandika historia mbaya kwa
shule? bila shaka hakuna, wadogo zangu nawaomba mzingatie masomo
achaneni na ngono kabisa muda wenu bado, huu ni muda wa kusoma" alisema
Mwakitalima
Kwa
upande wake Faustine Mwenda amewataka wanafunzi hao kujitambua kuwa
wamepelekwa shuleni kwa ajili ya kusoma hivyo wajisomee na watafaulu
vizuri hivyo kujijenge amsingi mzuri wa maisha pasipo kupata shida
Amesema
mafanikio yao yanajengwa na wao wenyewe hivyo endapo wataonesha uzembe
wa kupuuzia masomo ni dhahiri kwamba wataharibu malengo yao, hivyo
wanatakiwa kushika elimu na si mambo mengine yanayoweza kuwasababisha
wasifikie malengo yao ikiwemo kupata ujauzito.
Makete
girls ni sekondari pekee na ni mpya ya wasichana iliyoanzishwa mapema
mwaka huu wilayani hapo ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 36.Na Edwin Moshi, Makete.
No comments:
Post a Comment