Posted: 06 Feb 2013 01:27 AM PST
Mchuuzi wa Samaki, Bw. Aloyce Sebastian akimfunga samaki na mpira (rubber band) ili maji yasiingie katika mapezi, kama alivyokutwa kwenye Soko la Samaki la Kimataifa Feri, Dar es Salaam hivi karibuni. Wateja wengi huamini samaki mwenye mapezi mekundu kuwa ni salama kwa kitoweo. (Picha na Asia Mbwana) |
Posted: 06 Feb 2013 01:24 AM PST
Na Goodluck Hongo KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, amesema chama hicho kitatumia ngumu ya umma kupeleka hoja zote za wabunge zilizokataliwa bungeni kwa wananchi. Dkt. Slaa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, hakuna mahakama nyingine za kuwashtaki Spika wa Bunge Bi. Anne Makinda na Naibu wake, Bw. Job Ndugai. “Hakuna mahakama yoyote ya wananchi iliyowahi kushindwa, nasi tutapeleka hoja zote zilizozimwa na bungeni na Spika Makina pamoja na Naibu wake Ndugai kwa wananchi,” alisema Alisema chama hicho kilishatangaza mwaka huu ni wa nguvu ya umma hivyo kitendo cha Spika na Naibu wake kushindwa kuliongoza Bunge ambalo ndiyo linaisimamia Serikali kwakuzima hoja muhimu kwa masilahi ya nchi na Watanzania,wananchi watatoa hukumu kwa Serikali na CCM. “Wananchi wanashindwa kupata haki zao mahakamani, polisi na sehemu zingine na hivi sasa vitendo hivi vimehamia bungeni kwa kuzima haki za wananchi.“Ipo siku uvumilivu utakwisha na kujua kwa nini nchi za Rwanda na Burundi waliingia vitani...nchi hizi hazijaingia katika vurugu kwa kupenda bali kutokana na ukandamizaji kama huu,” alisema. Alisema mwaka 2011, aliwahi kusema Tanzania haitatawalika na kuitwa mchochezi lakini leo maamuzi ya Spika ni ya kukandamiza wananchi kwani hoja zilizozimwa ni kwa manufaa ya Watanzania ambapo Spika na Naibu wake, wanaongoza Bunge kwa chuki. Aliongeza kuwa, kutokana na hilo amewaagiza wabunge wote wa CHADEMA kutokwenda kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hadi Spika atakapoweka wazi rufaa 10 zilizokatwa na wabunge hao. Aliwataka wajumbe wote ambao watakwenda katika mabaraza ya kutoa maoni ya Katiba Mpya, watoe mani ya kutaka Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote cha siasa ili Bunge liweze kufanya kazi kwa niaba ya wananchi si kwa matakwa ya CCM. Dkt. Slaa alisema, hivi sasa viongozi wanaoliongoza Bunge hilo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa kupindisha kanuni za Bunge wazi wazi na kama zingefuatwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, angejiuzulu. “Samuel Sitta (Mbunge wa Urambo, mkoani Tbaora na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki), aliongoza Bunge kwa aibu pale alipotaka kupindisha sheria lakini Spika wa sasa na Naibu wake ni balaa zaidi,” alisema Dkt. Slaa. Alisema cham hicho kinawapongeza wabunge wote wa upinzania waliosimama bungeni kupinga maamuzi ya Spika na hiyo ndio njia pekee ya kutafuta haki za Watanzania. |
Posted: 06 Feb 2013 01:23 AM PST
Na Rehema Mohamed MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaaam, Machi 11 mwaka huu, inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa zaidi ya sh. milioni 100, inayowakabili vigogo wa Shirika la VUKA-Tanzania, linalohusika kuendesha miradi ya UKIMWI.Washtakiwa hao ni Mwenyekiti wa shirika hilo Bw. Adolf Mrema, Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala, Bi. Hilda Urassa pamoja na mshauri Bw. Straton Simon, ambao wanadaiwa kutumia fedha za miradi ya UKIMWI. Jana kesi hiyo ililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya utetezi ambapo washtakiwa hao, walijitetea mbele ya Hakimu Sundi Fimbo na kufunga ushahidi wao.Wakitoa utetezi wao, washtakiwa hao walikana kutumia isivyo halali fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Shirika la SAT-Tanzania. Kwa nyakati tofauti, washtakiwa hao walidai fedha hizo walizitumia kwa ajili ya matumizi ya ofisi kama dawa kwa ajili ya waathirika wa VVU, kuendesha semina na kulipa mishahara ya wafanyakazi wao. Hata hivyo, washtakiwa hao hawakuwa na nyaraka za kuthibitisha matumizi ya fedha hizo na kudai kuwa, nyaraka hizo zilichomwa moto na mwenye nyumba aliyewapangisha ofisi kwa kuwa waliifunga.Walidai mwenye nyumba baada ya kuona wamefunga osifi, aliamua kumpangisha mtu mwingine hivyo kutoa vitu vyao na kusababisha nyaraka zao kupotea na nyingine kuchomwa moto kama uchafu. Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 37 likiwemo la kugushi, wizi na matumizi mabaya ya fedha.Inadaiwa kuwa, washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Juni11,2006 hadi Desemba 2007, Temeke, Dar es Salaam. NYANYA |
Posted: 06 Feb 2013 01:20 AM PST
|
Posted: 06 Feb 2013 01:14 AM PST
Na Charles Mwakipesile, Mbeya MWENYEKITI wa Kanisa la Moravian nchini, Jimbo la Kusini, Mchungaji Clement Mwaitebele, mewataka wachungaji 14 ambao alitangaza kuwafukuza baada ya kukiuka kiapo chao cha utumishi Misheni ya Dar es salaam, kuondoka katika nyumba za kanisa.Akizungumza na Majira jana, Mchungaji Mwaitebele ambaye alionesha kukerwa na wachungaji hao kuvuruga amani ndani ya kanisa hilo kwa kujitangazia Halmashauri Kuu yao kinyume na Katiba, alisema uongozi wa kanisa umechukua hatua stahiki kwa watumishi hao kwa kuwa wasaliti katika jimbo mama. Alisema inashangaza wachungaji hao kudai hawaitambui mamlaka iliyowafukuza badara yake wanasubiri maelekezo ya uongozi wa Bodi ya Dunia (Unity Bord) ulio na Makao Makuu nchini Ujerumani hali inayoonesha kuwa, pamoja na usomi wao bado wameshindwa kutambua taratibu.“Kwa kuwa wameonesha kiburi cha kutoitambua mamlaka yangu kikatiba, natangaza rasmi kuwa kuanzia leo (jana), nimefuta ujio wa Bodi ya Dunia kuja nchini kuzungumzia tatizo hili kwa sababu tayari limekwisha hawana umuhimu wa kuja,” alisema. Mchungaji Mwaitebele alisema Ofisi la Dunia ni Makao Makuu ya Jumuia ya kanisa hilo kama ilivyo Umoja wa Mataifa ambao hauwezi kuingilia mambo ya ndani nchini Tanzania hadi unapopewa taarifa na uongozi wa nchi. “Sisi kama viongozi wa jimbo mama, hatuoni umuhimu wa hawa viongozi Bodi ya Dunia kuja kusikiliza mazungumzo kwa sababu tayari tumemaliza mgogoro uliokuwepo na taratibu za kisheria zinachukuliwa,” alisema. Aliwataka wachungaji hao kuhama mara moja katika nyumba za kanisa kwani hivi sasa si watumishi tena wa kanisa hilo kwa mujibu wa katiba baada ya kushindwa kulinda kiapo chao kilichowataka kuwa watii uongozi badala yake wanatumika kuleta mipasuko.Aliongeza kuwa, wao walifuata utaratibu wa kanisa wa kukaa mezani ili kusikiliza matatizo ya Misheni hiyo baada ya Sinodi ya eneo hilo kumuondoa madarakani aliyekuwa Mwenyekiti wao. “Wakati mazungumzo yakiendelea, Mwenyekiti huyo alitangza Halmashauri Kuu yake jambo lililoonesha wazi usaliti mkubwa katika kanisa,” alisema Mchungaji Mwaitebele.Aliwaonya Watunza Hazina wa kanisa hilo kuepuka kushirikiana na wachungaji hao kwa kuchukua fedha za matumizi yao binafsi kwani uongozi wake utawaburuta mahakamani kwa kosa la wizi wa fedha za umma jambo ambalo asingependa litokee. Alisema Mamlaka iliyowafukuza wachungaji hao ni halali ambayo ilichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Kanisa na hivyo madai kuwa walipaswa kufukuzwa kwa pendekezo la Askofu ni upotoshaji wawanaoufanya ili kuliyumbisha kanisa. |
Posted: 06 Feb 2013 01:13 AM PST
Na John Gagarini, Pwani MABAHARIA sita wanahofiwa kufa maji baada ya jahazi walilokuwa wakisafiria kwenye Habari ya Hindi kuzama.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei, alisema mabaharia hao walipanda jahazi la mizigo na walikuwa saba lakini mmoja ameokolewa. Alisema jahazi hilo linalofahamika kwa jina la Soweto, lilizama katika Visiwa vya Koma, eneo la Mwamba wa Chokaa, wilayani Mkuranga. “Usajiri wa jahazi hili bado haujafahmika na lilikuwa na shehena ya mbao na mirunda likitokea Kyasi kwenda Zanzibar,” alisema.Aliwataja baadhi ya mabaharia wanaohofiwa kufa maji kuwa ni Ally Hasan, Hassan Mamba, Nasoro Isa, Abdala Said na Husein Huku wakati Hasan Rajab, aliokolewa na wanaendelea kutafutwa.Aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kawa wataziona maiti zinazoelea majini. |
Posted: 06 Feb 2013 12:57 AM PST
Na Godfrey Ismaely, Manyara WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, amesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kuona matukio ya ujangili nchini yanaongezeka siku hadi siku, muda wowote ataagiza majeshi yote kushirikiana ili kudhibiti matukio hayo.Hatua hiyo inatokana na Serikali ya Tanzania kusaidi dikezo maalumu na Serikali ya Marekani ambalo kushirikiana katika kudhibiti matukio ya ujangili nchini.Balozi Kagasheki aliyasema hayo jana mkoani Manyara katika hafla maalumu ya uzinduzi wa Kituo cha Mapokezi kwa watalii ambacho kipo chini ya Jumuiya ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyapori Burunge (WMA), Wilaya ya Babati, mkaoni Manyara, kilichojengwa na Marekani kupitia Shirika lake la USAID. Jana (juzi) mimi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Bw. David Hayes, tulisaini dokezo hili kwa lengo la kukomesha matukio ya ujangili nchini,” alisema na kuongeza kuwa, matukio ya ujangili yanaichafua nchi pia ni mateso kwa wanyama.Alisema mapambano dhidi ya majangili yanawezekana ambapo Serikali imeanza kujipanga ambapo Rais Kikwete, wakati wowote atatoa uamuzi kamka Amiri Jeshi Mkuu wa nini kifanyike kudhibiti hali hiyo nchini. Alisema suala la kucheleweshwa fedha zinazotokana na makusanyo ya WMA ambayo ni asilimia 50 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi, litafanyiwa kazi na wakati wowote mambo yatakuwa mazuri.Kwa upande wake, Bw. Hayes ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, alisema lengo la nchi yake kutoa ufadhiri kwa jumuiya za WMA nchini, mbali ya kulenga kukomesha ujangili pia jamii zitanufaika kupitia mapato mbalimbali. “Kufanikiwa kwa WMA ni fursa moja wapo ya kukomesha kabisa matukio ya ujangili yanayotokea Tanzania, vitendo hivi vinachangia kuhatarisha usalama wa binadamu, wanyamapori na hata kutatiza shughuli za utalii,” alisema Bw. Hayes.Balozi wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt's, alisema utaratibu wa wanajamii kuanzisha WMA nchini umeweza kuwa na mafanikio makubwa, kuboresha miradi ya shule, zahanati na kusomesha watoto kutokana na mapato yanayopatikana kutoka kwa wawekezaji walioingia nao mikataba. “Tangu mwaka 2006, WMA tisa zimeweza kuingia mikataba na wawekezaji binafsi katika sekta ya utalii ambapo zimefanikiwa kupokea zaidi ya dola za Marekani milioni tano kutokana na shughuli za uwindaji na upigaji picha. “Hatua hii imewezesha zaidi ya wanajamii 400,000 kunufaika kwa namna moja ama nyingine pamoja na kupata ajira hivyo Marekani itaendelea kuzijengea uwezo jumuiya hizi mara kwa mara ziweze kufikia malengo ya uhifadhi na maendeleo kwa wananchi,” alisema. MADAFU |
Posted: 06 Feb 2013 12:52 AM PST
|
Posted: 06 Feb 2013 12:48 AM PST
Na Masau Bwire, Bunda OFISA Mtendaji wa Kata ya Iramba, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, Bw. Simon Katikizu, amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumshambulia kwa mawe wakimtuhumu kuiba mahindi ya msaada. Tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Kijiji cha Isanju ambacho ni Makao Makuu ya kata hiyo ambapo wananchi walikusanyika ili kugawiwa mahindi ya msaada.Wakati kazi ya kugawa mahindi hayo ikiendelea, wananchi hao walibaini upotevu wa magunia zaidi ya 40 na baada ya kufanya uchunguzi, wakagundua wizi huo ulifanywa na Bw. Katikizu hivyo walianza kumshambulia kwa mawe na marungu. “Tumemkamata na mahindi ya msaada akiwa ameyaficha nyumbani kwake, katika Ofisi ya Elimu, kilimo na mengine aliyaweka katika nyumba za rafiki zake, wakati akijaribu kukimbia lilipigwa yowe,” alisema Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, katika kata hiyo, Bw. Mohamed Gamba.Alisema Serikali ilipeleka msaada wa magunia 318 ya mahindi kwa ajili ya vijiji vitano vya kata hiyo ambapo kila kijiji kilipaswa kupata magunia 63 kutokana na njaa inayowakabili wananchi. Vijiji vilivyokumbwa na tatizo la njaa ni Isanju, Mugara, Sikiro, Nyarugoma na Mwiruruma, lakini Bw. Katikizu aliiba kiasi kikubwa cha mahindi ambapo kijiji cha Nyarugoma, kiliambulia magunia 26 ndipo wananchi walipokuja juu na kugundua wizi huo. Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Joshua Mirumbe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa, tayari amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri amsimamishe kazi Bw. Katikizu kwa kosa hilo. “Huyo Ofisa Mtendaji habari zake ninazo, aliwahi kuiba na kuuza mitumbwi 20 iliyokamatwa katika uvuvi haramu hivyo kutokana na tukio hili, nimeagiza Mkurugenzi amsimamishe kazi kuanzia leo (jana) na ashitakiwe kwa wizi,” alisema Bw. Mirumbe.Alisema viongozi wa namna hiyo hawafahi kuendelea kuongoza na wanaitia doa Serikali hivyo hawana budi kuondoka wabaki viongozi waaminifu na waadilifu watakaowaletea wananchi maendeleo. “Siko tayari kuona viongozi wezi, wabadhilifu na wababaishaji wakiendelea kuwanyonya wananchi kwa kuwaibia, kama wapo wajiondoe kabla sijawafikia, nitaanza na huyo Ofisa Mtendaji ili iwe mfano kwa wengine,” alisema.Majira lilipomtafuta Bw. Katikuzu na kumuuliza juu ya tuhuma hizo alidai madai hayo ni uzushi uzushi na hakuna wizi wowote aliofanya bali yeye ni miongoni mwa Watendaji waadilifu wilayani humo wanaoaminiwa kiutendaji na Bw. Mirumbe. |
Posted: 06 Feb 2013 12:41 AM PST
Na Miriam Sarakikya
BAADHI ya wananchi wanaoishi mabondeni eneo la Tegeta kwa Ndevu, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wameiomba Serikali iwasaidia kuwapa viwanja ili waweze kuondoka katika maeneo hatarishi kutokana na kero wanayopata kipindi cha mvua.Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti Dar es Salaam juzi, wananchi hao walidai wanashindwa kuondoka maeneo hayo kutokana na ukata wa fedha za kununulia viwanja. “Baadhi yetu wamejenga nyumba zao katika maeneo haya na wengine wamepanga, tunaiomba Serikali isikilize kilio chetu ili tuweze kuhamia maeneo salama tofauti na sasa kwani tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,” alisema mkazi wa eneo hilo Bw. Edgar Msanganzila.Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema hivi sasa eneo lao linafurika maji kutokana na mto uliopo jinani na makazi yao hivyo kuhatarisha maisha yao na familia zao. Hivi karibuni wananchi hao waliitisha mkutano wa hadhara na kukubaliana kuupanua mto huo maarufu 'Mto Tegeta', ili kupata njia ya kupitisha maji kirahisi pindi mvua zinaponyesha lakini hadi sasa mpango huo haujafanikiwa. Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 |
Posted: 06 Feb 2013 12:40 AM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu fedha zake.Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma na kumpiga nacho marehemu kichwani. “Adhabu ya kuua bila kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema. Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na amekiri kosa. Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw, mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi, Manispaa ya Dodoma. |
Posted: 06 Feb 2013 12:38 AM PST
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tarakea, mkoani Arusha, Bw. Martin Kija (kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Bw. Masaki Okada wakitia saini makubalino, Dar es Salaam jana, ambapo Serikali ya Japan itajenga mabweni ya wasichana ya shule hiyo. Ujenzi wa mabweni hayo utawaondolea tatizo la kutembea umbali mrefu kutoka maeneo wanayoishi. (Picha na Asia Mbwana) |
Posted: 05 Feb 2013 10:33 PM PST
Na Pendo Mtibuche, Dodoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dodoma, juzi ilimuhumuku mkazi wa Dodoma Mjini, Yohana Chipini (23), kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Alord Ndeshio, bila kukusudia wakati akidai sh. 4,000. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary Shangali baada ya mshtakiwa kukiri kosa na kumtia hatiani. Jaji Shangali alidai kuwa, amezingatia maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka pamoja na utetezi kuhusu chanzo cha mauaji hayo ambacho ni ugomvi uliotokea kati yao wakati mshtakiwa alipokwenda kumdai marehemu fedha zake. Aliongeza kuwa, baada ya ugomvi huo mshtakiwa aliokota kipande cha ubao au kitu kinachoaminika kuwa kipande cha chuma na kumpiga nacho marehemu kichwani.“Adhabu ya kuua bila kukusudia ni kifungo cha maisha lakini kutokana na mazingira yalivyoonyesha na utetezi wa mshtakiwa, Mahakama imempunguzia adhabu na hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani,” alisema. Kabla ya hukumu hiyo, wakili wa mshtakiwa, Steven Kuwayawaya, aliiomba mahakama impunguzie adhabu mshtakiwa akidai kosa hilo ni la kwanza na amekiri kosa.Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuw, mshtakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2012 katika barabara ya Bahi, Manispaa ya Dodoma. |
Posted: 05 Feb 2013 10:30 PM PST
Na Mariam Mziwanda MAOFISA Kilimo zaidi ya 20 kutoka Wilaya tano nchini, wapo kwenye mafunzo ya mradi shirikishi wa kupunguza wimbi la viwavi jeshi ambavyo ni kero sugu kwa wakulima na kusababisha njaa katika baadhi ya maeneo nchini.Akizungumza katika mafunzo hayo Dar es Salaam juzi, mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Ofisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kanda ya Kaskazini, Bw. Didas Moshi alisema mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuwatambua na kuwaangamiza kabla ya kukua. “Tumeanza mafunzo haya na Wilaya tano ambazo ni Kisarawe, Nachingwea, Masasi, Lindi Vijijini na Kilwa, mafunzo haya yanaendeshwa kwa msaada wa watu wa Marekani ambao wameona viwavi jeshi ni kero kwa wakulima,” alisema.Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Mimea kutoka katika Wizara hiyo, Cornelius Mkondo, alisema mazao mengi ya wakulima nchini yamekuwa yakiathiriwa na milipuko ya wadudu sugu wanaoshambulia mazao kwa haraka.Alisema viwavi jeshi wamekuwa wakipoteza nguvu kazi za wakulima hivyo imeamua kutafuta mbinu za kuwatokomeza. Aliongeza kuwa, maofisa hao watafundishwa mambo mengi hususan jinsi ya kufahamu mlipuko unavyotokea na kuimarisha mawasiliano kati ya vijiji, kata, Wilaya hadi Taifa.“Lengo ni kujilinda na viwavi, katika kuhakikisha operesheni hii inakuwa endelevu, tutashirikiana na kampuni za simu ili wakulima waweze kufahamu utabiri wa hawa wadudu waharibifu,” alisema na kuongeza kuwa, mradi huo mbali ya Tanzania pia unaendeshwa katika nchi za Kenya na Ethiopia. |
Posted: 05 Feb 2013 10:29 PM PST
Na Rose Itono WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekabidhiwa majukumu ya kuweka viwango vya ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za elimu kuanzia awali mpaka sekondari.Sambamba na hilo wizara pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa elimu ya awali,msingi,sekondari na ile ya watu wazima inatolewa kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika. Wizara pia ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa utoaji wa elimu kwa kufanya ufuatiliaji na tathmini pamoja na kufanya mapitio,kuandaa na kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Sera, Mipango, Sheria na kanuni za elimu zilizopo,kulingana na mabadiliko ya dhima na dira ya Serikali huku ikiandaa mikakati ya utekelezaji wake. Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya taaluma katika ngazi zote za elimu na mafunzo.Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatekeleza mipango mbalimbali ili kuinua ubora wa elimu Ili yote hayo yaweze kufanikiwa juhudi za wazazi na walezi kwa kushirikiana na wanafunzi zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika kuleta matokeo mazuri.Nimeongea hivyo kwa makusudi kwani kumekuwa na baadhi ya wazazi,walezi ambao wamekuwa wakiwakatisha masomo wanafunzi hasa wa kike kwa kutaka kuwaoza kwa nguvu kwa nia ya kujipatia fedha ama mali. Nionavyo kwa kufanya hivyo kutalipunguza tatizo la wazazi ambao wana tamaa za kujipatia pesa kwa mahari kupitia watoto wao bila kuangalia madhara na vitu vya msingi ambavyo mtoto wa kike atavikosa kutokana na kuolewa bila kuwa na elimu. Hivi karibuni tumeshuhudia mtoto wa kike ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Tongani kata ya Mkaramo wilayani Pangani akitoroka kwao na kukimbilia kujificha porini akikwepa kuachishwa shule.Nionavyo hali hii ni hatari kiusalama kwa mtoto huyo ambaye angeweza kupata madhara ya kukutana na wanyama wakali na hata kupoteza maisha.Hali ya mtoto huyo kuamua kulala porini ilimuwezesha kufika kwa Mkuu wa Wilaya ya handeni kuomba msaada ambao utamuwezesha kuweza kuendelea na masomo. Nionavyo kulingana na hali hiyo ni wanafunzi wangapi wenye ujasiri kama aliouonyesha msichana huyo ambaye aliamua kujitoa muhanga na kuamua kulala porini ili kukimbia kuolewa.Kwa maelezo ya mtoto huyo anasema aliamua kukimbilia kwa Mkuu wa Wilaya baada ya kusikia kuwa kuna mradi wa 'Niache Nisome' ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumkomboa mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utotoni. Nionavyo kwa mfano wa mradi huu ni wazi serikali ikaona umuhimu wa mradi huo kusambaa nchi nzima ili kuwawezesha vijana wa kike kujikomboa na ndoa na mimba za utotoni. |
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, February 7, 2013
UTUNZAJI CHADEMA kuwashtaki Makinda, Ndugai *Dkt. Slaa adai wameshindwa kuliongoza bunge Hukumu ya vigogo Shirika la VUKA kutolewa Machi 11 NYANYA Mgogoro Moravian wachukua sura mpya Mabaharia 6 wahofiwa kufa maji Serikali yajipanga kukomesha ujangili nchini MADAFU Mtendaji anusurika kifo akidaiwa kuiba mahindi Wakazi waishio mabondeni Tegeta waomba viwanja Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 MKATABA Jela miaka 2 kwa kuua akidai sh. 4,000 Wapema mafunzo kupunguza viwavi jeshi Mradi wa 'Niache Nisome' usambazwe nchi nzima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment