Alisema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
inajengwa katika mfumo wa ushindani wa soko na kwamba kila fursa iliyopo
katika Jumuiya inapatikana kwa ushindani miongoni miongoni mwa wananchi
wa nchi wanachama.
"Hivyo, Watanzania kama raia wa nchi zingine wanachama ni lazima
wachangamkie fursa na kuzitumia. Ili kushindana, Watanzania wanatakiwa
kujiamini na kuacha kujiona wanyonge ndani ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwani akili tunazi, uwezo tunao na nguvu tunazo," alifafanua.
Akichangia katika mkutano huo, Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan
Kiula, alisema ni vema elimu kuhusu mtangamano wa Afrika Mashariki,
hususan kuhusiana na fursa za kibiashara, ikatolewa pia kwa wafanyakazi
wa taasisi zinazofanya kazi kwenye maeneo ya mipakani, kama vile Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa kikwazo kwa
wafanyabiashara kutokana na utendaji wao usioridhisha.
Alisema watumishi katika vituo vya mipakani wamekuwa wakiwakatisha tamaa
wananchi wanaofanya biashara kiasi cha kuwafanya waendelee kutumia njia
za panya.
Naye mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema) alisema Tanzania
bado ina kazi kubwa katika ushindani ndani ya Jumuiya akitolea mfano wa
Kenya ambayo imefikia uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda vya kutosha
wakati nchi yetu ndio inafikiria kufufua na kuanzisha viwanda.
Alisema kuna hatari ya Tanzania kubakia kuwa soko wakati nchi kama Kenya
zinapambana kufanya uzalishaji mkubwa wa viwandani na kuimarisha ubora
wa bidhaa zake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi
Rajabu aliwataka Watanzania kutafuta mbinu za kuwa wabunifu zaidi katika
ushindani ndani ya Jumuiya ili kuweza kufanikiwa kukamata fursa za
mtangamano.
Wabunge wa Afrika Mashariki ambao wapo katika shughuli za kuhamasisha na
kuelimisha umma kuhusu fursa za mtangamano wa Afrika Mashariki wamesema
siku za usoni wanatarajia kufanya mkutano na wabunge wote ili
kubadilishana nao uzoefu kuhusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania,
(EALA), Makongoro Nyerere akifafanua jambo wakati wabunge kutoka EALA
walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama
pamoja na Kamati ya Viwanda Biashara na
Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kadumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalali Kafumu. (Picha
na Francis Dande)
No comments:
Post a Comment