TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 12, 2016
KIJIJI CHA OLBILI CHAKABILIWA NA NJAA.
Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.
Na Woinde Shizza,Simanjiro.
KIJIJI cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai
wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kinakabiliwa na tatizo la ukosefu
chakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota
kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.
Wananchi wa kijiji hicho Zuhura Salim na Anna Lazaro wamesema kuwa
uhaba huo wa chakula unatokana na kunyang`anywa maeneo waliyokua
wanatumia kwa kilimo na kutumika kama ardhi ya malisho.
Wananchi hao waliandamana na mabango yao kuzunguka eneo la shamba hilo
wameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi na wizara ya kilimo
kuingilia kati mgogoro huo baina yao na wafugaji wanaogombea eneo hilo
ambalo kwa zaidi ya miaka 24 tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2013 ambapo
walizuiwa kutumia maeneo hayo ambayo walikua wakiyatumia kwa
shughuli za kilimo cha kujikimu.
Eliud Jackson ni Mwanakijiji wa Olbili amesema kuwa licha ya kunyimwa
maeneo ya kulima pia mwaka huu hawakupata chakula cha msaada kama kata
nyingine zilizopata mgao huo hivyo kuteseka na njaa wao na watoto wao
,wamemuomba Rais Magufuli kutazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tilili Kingi Lomayani Laizer amesema kuwa
baada ya kuzuiliwa kulima na Mtendaji wa Kata na Diwani aliyekua
madarakani walifika katika ngazi za wilaya bila mafanikio hivyo
wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Manyara afike kutatua mgogoro huo ili
kuwanusuru na baa la njaa.
“Nimefuatilia suala hili kwa Mwenyekiti,Mtendaji wa kata na Diwani
aliyemaliza muda wake bila mafanikio kwani wao ndio walitoa zuio la
kutuzuia kulima katika maeneo haya ,inaonekana jambo hili
linashikiliwa na wafugaji wenye fedha wanatumia fedha zao kuwanyanyasa
wakulima” Alisema Laizer
Aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo,ardhi kufika katika kijiji
hicho na kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwani wamekua wakishindwa
kuendesha familia zao kutokana na kutegemea kilimo kama shughuli ya kuwapatia chakula na kipato.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment