Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016
ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa
Singida Marehemu Christina Lissu Mughwai
katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
Christina Lissu
Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha
kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika
hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.
Pamoja na Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli
ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Akitoa salamu kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa
katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa
mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.
"Mheshimiwa
Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki
wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake
lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa
Simbachawene.
Mwili wa Marehemu
Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida
kwa Mazishi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
12 April, 2016
No comments:
Post a Comment