TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 12, 2016
MAAFISA WA JWTZ WAMALIZA MAFUNZO KENYA.
Balozi Haule (Katikati) akimpongeza Mwambata wa Kijeshi Ubalozini Nairobi, Luteni Kanali Fabian Machemba. Kulia ni Kanali Msola.
Balozi Haule akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha ziara ya Maafisa wa JWTZ.
Maafisa na wanafunzi 29 kutoka Chuo cha Kamandi na Unadhimu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Duluti, Arusha, wamemaliza ziara ya mafunzo ya wiki moja nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita, iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).
Kundi hilo lililoongozwa na Naibu Kamanda na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha JWTZ, Kanali Celestine Msola, lilitembelea taasisi mbalimbali za serikali na Jeshi la Kenya pamoja na taasisi binafsi. Mafunzo yao yalihusu masuala ya Jamii na Uchumi, Utawala bora, Mfumo wa Kisiasa, Ulinzi na Usalama, na Maendeleo ya Teknolojia ya Kivita.
Akizungumza katika hafla fupi mwishoni mwa ziara hiyo, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, alimshukuru Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Samson Mwathethe, na watendaji wake, kwa ukarimu waliowafanyia Maafisa wa JWTZ.
Aliwapongeza Maafisa hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoonyesha muda wote, akisema wameacha sifa nzuri ya JWTZ na Tanzania kwa ujumla.
Mwakilishi wa KDF, ambaye pia ni Kamanda wa Chuo cha Teknolojia cha Ulinzi, Kanali Oscar Muleyi, alisema Maafisa wa Jeshi la Kenya wameshafanya ziara ya mafunzo nchini Tanzania na walikarimiwa vizuri sana.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment