TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Tuesday, April 12, 2016
Airtel yaleta 'Jipimie Yatosha Yako' kutoa uhuru zaidi vifurushi vya Yatosha
Airtel Tanzania ili kutoa uhuru zaidi kwa wateja wake imetangaza kifurushi kipya kupitia huduma yake ya vifurushi vya Airtel Yatosha kijulikanancho kama Airtel Jipimie Yatosha Yako itakayowapa wateja wake faida kubwa na uwezo wa kuweza kupanga na kuunda kifurushi wanachokitaka kutokana na chaguo na mahitaji yake .
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Anethy Muga alisema "Jiunge sasa na Airtel ufurahie Uhuru huu mpya, Tumezindua " Airtel Jipimie Yatosha Yako " kwa ajili ya kuwapatia wateja wetu uhuru wa kuchagua na kupanga matumizi yao na papo hapo kuunda kifurushi kitakachoweza kukidhi mahitaji yao ya kiuchumi na kijamii.
Airtel Jipimie Yatosha Yako "ni moja ya kifurushi cha kibunifu zaidi ambacho na kinapatikana kwa wateja wetu wote hapa nchini ambapo unaweza kupata kifurushi hiki upendavyo wewe yaani kwa siku, wiki, na hata mwezi.
“Airte daima tunafanyia bidhaa zetu zote utafiti na kuziunda kwa mujibu wa kile wateja wetu wanataka ili kuleta unafuu na ubora zaidi, kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wateja wa simu za mkononi wa Airtel wataweza kuamua kununua vifurushi vya gharama nafuu na watakavyo vya hadi shilingi 500 huku wakijipimia muda wa maongezi tu, au changanya na MB zaidi au unajichaguali Muda wa maongezi na SMS au kujipimia vyote yaani Muda wa maongezi Zaidi, MB zaidi na SMS Zaidi, uhuru ni wako kujipimia utakavyo” na sasa ndio wakati wa kujiunga na Airte.
Airtel inaamini ubunifu wa huduma ya “Jipimie Yatosha Yako" itakuwa suluhisho la mawasiliano kwa wengi na msaada kwa wale ambao walitaka kifurushi kutokana na hitaji lake. Sasa wateja wa Airtel wanauwezo wa kutengeneza Yatosha yao wao wenyewe na kutimiza mahitaji yao .
Kujiunga na kifurushi cha Yatosha na kufurahia Jipimie Yatosha Yako, wateja wanatakiwa kupiga namba *149*99# na kuchagua namba 5 ‘Jipimie Yatosha Yako’ na kutengeneza kifurushi cha chaguo lake.
Huduma mpya ya uhuru wa kujipimia Vifurushi vya Yatosha imezinduliwa na kusindikizwa na wasanii wa kundi la Navy kenzo linaloundwa na Nahreel na Haika ambao wataitambulisha sehemu mbalimbali nchini
“Sisi tuko tayari kama kawaida kuja kujipimia yatosha kila mahali, sasa na nyie kuweni tayari kukamatia chini Yatosha yako inayokutosha" alisema Nahreel wa Navy Kenzo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment