TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Sunday, April 10, 2016
HOSPTALI YA RUFAA IRINGA YAPEWA MWEZI MOJA KUTAFUTA UFUMBUZI WA UTEKETEZAJI WA TAKA HATARISHI
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa Iringa Bw. Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja wakifanya usafi katika soko la mji wa Iringa.
Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi sokoni Mkoani Iringa Leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, Akiuandaa mche wa mti kabla kuupanda katika eneo la chanzo cha maji cha chemchem cha Kitwiru, Leo Mkoani Iringa.
Kulia Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake walipokagua mazingira ya hosptali hiyo leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Akimwagilia maji mara baada ya kupanda mti , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa Kulitaftia ufumbuzi suala la uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.
Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa maziringa katika viwanda vya mkoa wa Iringa.
Imeelezwa kuwa uteketezaji wa tanga hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote uliosababishwa na taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.
Kwa Upande wake mganga mkuu mfawidhi wa hospital hiyo dkt Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina kuwa taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la mkoani hapo na hata hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za sindano, gloves, nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.
Akitolea ufafanunuzi sualala za uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza limewahi kushauri uongozi wa hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia kuziharibu.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo Mh. Mpina,alipanda mti katika kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake na kuwaasa watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwivu.
“Taifa lazima lipande miti ili kuhepukana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini na tano kwa mwaka.
MPALULEBLOGS:
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment