TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, April 16, 2016
WANYAMA PORI WAVAMIA MASHAMBA YA WANANCHI NA KUMALIZA MAZAO YAO
Na Woinde Shizza,Karatu
Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.
Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.
Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua zozote ambazo wamezichukuwa.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.
Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye amechukuwa hatua .
“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja nakutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada yakutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizolililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katikakituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezikuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyajeunakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache aleakitosheka aondoke “alisema Seuri lazier
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment