TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, April 16, 2016
MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU LILILOANDALIWA NA RAIS BARACK OBAMA
.Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho lililoandaliwa na Rais Barack Obana na kufanyika White House April 13. 2016.
.Mwanafunzi Armo Halwan akimuelekeza Rais wa Marekani,Barack Obama anavyoweza kutumia simu kuendesha cha kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya Jijini New York kupitia timu yao ya ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni Wendy Ni na anayefuatia ni Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha namna gani kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za ardhini ( Subways).
Stephen Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu kuendesha mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya Rais ( White House Science Fair 2016)
Rais Barack Obama akipeana mkono na Stephen Mwingira na timu yake baada ya kumaliza kutoa maelezo yao kifaa walichokibuni. Kwa miaka sita Rais Barack Obama amekuwa akifadhili maonyesho ya ubunifu wa vifaa mbalimbali vilivyobuniwa na wanafunzi kuanzia wale wa shule za wali hadi sekondari ikiwa ni jitihada zake za kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, teknolojia na hesabu tangu wakiwa wadogo na hivyo kuibua vipaji vyao. katika onyesho hilo la mwisho wa utawala wa Barack Obama jumla ya wanafunzi 130 kutoka states mbalimbali walishiriki.
Stephen Mwingira akiendelea kutoa maelezo zaidi kwa Rais Obama namna kifanya cha kufanyia usafi kwenye njia za reli ambacho ni cha gharama nafuu kinavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment