Kituo
cha EFM redio kwa mara nyingine tena kimeibuka na shindano lake la
shika ndinga kwa mashabiki wake wa jiji la Dar na Pwani. Pamoja na
kufanyika kwa shindano hilo lililozua msisimko mkubwa miongoni mwa
wilaya ya Temeke,EFM Radiao pia waliwatangaza watangazaji wao Wapya
watatu waliokuwa Clouds FM,Watangazaji hao ni Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando.Shindano hilo Kwa mwaka huu ,limezinduliwa rasmi jana April 9/2016 kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo alisema kuwa shindano hilo litaendelea pia kwa wilaya ya Ilala, Kinondoni, Bagamoyo, na Kibaha na hatimae kilele chake kufanyika katika uwanja wa Sinza TP.
Sebo alisema kuwa Shindano hilo litaanza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia kwenye fainali ya kujinyakulia gari ambao wamepata nafasi ya kushiriki kwa njia ya kupiga simu na kujibu kiufasaha swali husika ili kupata nafasi ya kushiriki shindano la shika ndinga. Alisema kuwa shindano hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali.Lengo ni kuwawezesha wasikilizaji wake kwa namna moja ama nyingine katika kuongeza na kukuza kipato kitakacho changia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.

No comments:
Post a Comment