Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi
wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji
vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui wakati Waziri huyo
alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi
katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora
Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa
Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
PICHA
na GCU – HAZINA
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na
viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi wa vijiji vya Milenia wa
Mbola jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu
kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo
8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano
ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo.
Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na
kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
…………………………………………….
Na
Mwandishi wetu -GCU-Hazina- Uyui- Tabora
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa
amewataka wakazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora waliopo katika wa
utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola
kuufanya mradi huo kuwa endelevu kwa kutunza vizuri miradi yote iliyoibuliwa
kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya wananchi wa eneo hilo .
Waziri
huyo alitoa kauli hiyo jana wilayani Uyui mkoani Tabora mara baada ya kuzindua
maabara iliyochini ya mradi huo ambayo imegharimiu shilingi milioni 49 hadi
kukamilika.
Alisema
kuwa ni vema wananchi hao wakahakikisha miradi yote iliyotekelezwa chini ya
mradi wa vijiji vya milenia wa Mbola inatunza vizuri ili iwe darasa la
kufundishi vijiji vingine hapa nchini katika utekelezaji wa malengo 8 ya
milenia.
Dkt.
Mgimwa aliongeza kuwa itasikitisha kuona kuwa mara baada ya muda wa mradi kuisha
wa 2006-2012 na wafadhili ambao ni Milenia Promise Tanzania kumaliza muada wao
na miradi inakufa na kusema kuwa hatua hiyo haitakuwa nzuri.
Aidha
alitoa wito kwa wanavijiji wengine ambao hawapo katika mradi huo kwenda katika
Kijiji cha Ilolanguru wilayani Uyui ili wajifunze jinsi ya utekelezaji wa
malengo ya Milenia kwa kutumia juhudi za wananchi.
Awali
akitoa taarifa kwa Waziri wa fedha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally
Magoha alisema kuwa katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa
vijiji vya Milenia wa Mbola wameweza kuboresha maisha yao katika vijiji 16
katika eneo hilo.
Alitaja
manufaa waliyokwishapata ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa kutumia
matofali ya kuchoma na bati na kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na fedha.
Mogoha
aliongeza kuwa pia mradi huo umewawezesha kupunguza tatizo la vifo vya watoto
waliopo chini ya maika 5 na mamawajawazito ambapo awali vifo vilikuwa wastani
wa watoto watatu(3) hadi watano (5) na wanawake wajawazito 3 hadi 5 katika
kipindi cha miezi mitatu lakini hivi sasa vifo ni wastani huo katika kipindi
cha miezi sita na wakati mwingine hakuna.
Alisema
kuwa hatua hii imefikiwa mara baada ya kuwaelimisha wananchi juu ya kutumia
vyandarua na kuua mazalia ya mbu na hivyo kupunguza malaria katika eneo hilo.
vilevile
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kiwango cha wanafunzi wanaoishia njia(drop out)
kimepungua mara baada ya mradi huu kuanza kwani mbinu mbalimbali zimesaidia
watoto wengi kumaliza darasa la saba .
Mbinu
hizo ni pamoja na kutoa chakula kwa wanafunzi na kuhamasisha michezo mashuleni
jambo liliwavutia watoto wengi.
kuhusu
suala la maji alisema wanaendelea vizuri ambapo wastani wa asilimia 60 ya
wakazi wa eneo hilo wanapata maji safi na salama.
Mradi
wa vijiji vya Milenia wa Mbola unatelelezwa katika vijiji vya Ilolanguru,
Isenga, Ngokolo, Ulimakafu, Mpenge, Isila, Mbola, Kasisi A, Mabama, Ideka,
Mbiti, Msiliembe, Iberi, Inonalwa, Usagari, Msima na Migungumalo.
No comments:
Post a Comment