Mchezaji Kasey Keller wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani.
Aliyekuwa Kipa Marc Burchklabu ya Seattle Sounders ya Marekani
………………………………………………………………………
WAWAKILISHI wawili wa klabu ya
Seattle Sounders ya Marekani wataendesha semina kwa wadau wa michezo
hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch na kipa aliyestaafu ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .
Wakiwa nchini, wachezaji hao
wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za
msingi katika siku na muda ambao utangazwa hapo baadaye. Z
iara hiyo ni moja ya kukuza
ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau wa michezo nchini na
ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania,
Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester
United.
Kwa kushirikiana na Washington
Global Health Alliance (WGHA), wawakilsihi wa timu hiyo pia
watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha
ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH na Chuo kijulikanacho kwa
jina la Washington State University’s Paul G. Allen School for Global
Animal.
”Ziara hii itadumisha na
kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “ alisema Mmiliki wa
timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March watakuwa mabalozi
wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.
Alisema kuwa wajumbe hao pia
watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro Crater na jiji kubwa la
Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani iliingia katika
ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la kushughulika na
masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.
No comments:
Post a Comment